Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE MAPIGANO

Ukraine: Rais Volodymyr Zelensky amewafuta kazi maofisa wa umma

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfukuza kazi mwendesha mashtaka mkuu nchini humo Iryna Venediktova pamoja na mkuu wa usalama Ivan Bakanov hatua anayosema imehusishwa na uhaini unaotekelezwa na maofisa wake wa usalama.

Volodymyr Zelensky, rais wa Ukraine.
Volodymyr Zelensky, rais wa Ukraine. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa taifa, Zelensky amesema kuwa maofisa 60 waliosalia katika maeneo yanayokaliwa kwa sasa na Urusi wanafanya kazi kwa kushirikiana na Moscow dhidi ya Ukraine.

Rais Zelensky aidha amesema kuwa mamlaka nchini mwake inachunguza zaidi ya visa 650-vinavyohusishwa na uhaini pamoja na kutoa msaada kwa adui wa Taifa Lake.

Tangazo lake likija wakati ambapo pia mawaziri wa mambo ya nje katika mataifa ya EU wanapokutana kujadili hatua ya kutangaza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi, ikiwemo uwezekano wa kupiga marafuku uwagizaji wa dhaabu kutoka nchini humo.

Hadi sasa EU imetangaza vikwazo sita dhidi ya Ursui. Mwezi Juni EU ilitangaza vikwazo dhidi ya uwagizaji wa bidhaa za mafuta kutoka nchini humo.

Kando na kulenga bidhaa za dhaabu, Muunganao huo pia unawazia kutangaza vikwazo dhidi ya maofisa zaidi katika serikali ya Moscow.

Ursula von der Leyen raisΒ wa kamishena ya EU katika taarifa yake ameeleza kuwa Moscow lazima iendelee kuadhibishwa vikali kutokana na kuendelea kuivamia Kyiv.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.