Pata taarifa kuu
UFARANSA-AUSTRALIA

Australia na Ufaransa zakubaliana kuimarisha tena uhusiano wao

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese katika kikao na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron jijini Paris, amekaribisha uhusiano mpya kati ya nchi hizo mbili, baada ya mwaka uliopita nchi yake kusitisha mkataba wenye thamani ya Euro Bilioni 33 kuuziwa manuari ya kivita, ilikuwa imeitoa kwa Ufaransa na kutikisa uhusiano wa kidplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, akiwa na Waziri Mkuu wa Australia  Anthony Albanese, walipokutana jijini Paris
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, akiwa na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, walipokutana jijini Paris AP - Thomas Padilla
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo mpya wa Australia amesema amekuja jijini Paris, kujenga uaminifu na kuheshimiana kati ya nchi hizo mbili.

Macron naye amesema, serikali mpya ya Australia imeonesha kuwa, kuna uwezekano wa nchi hizo mbili kushirikiana kwa kuheshimiana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.