Pata taarifa kuu

Nchi za Ulaya zapiga marufuku uingizaji wa mafuta kutoka Urusi

Viongozi wa mataifa ya Ulaya, wamekubaliana kuzuia uingizaji wa  bidhaa za mafuta kutoka Urusi kwa asilimia 90 kufikia mwisho wa mwaka huu, kama shinikizo za kuitaka kuacha vita nchini Ukraine. 

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel akiwasili katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya kujadili vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Mei 30, 2022 mjini Brussels.
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel akiwasili katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya kujadili vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Mei 30, 2022 mjini Brussels. REUTERS - JOHANNA GERON
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya makubaliano kati ya viongozi hao, waliokutana jijini Brussels, baada ya kuwepo kwa pingamizi kwa nchi ya Hungary. 

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya Charles Michel amearifu kupitia ukurasa wa Twitter kuwa wakuu wa nchi 27 wanachama wa umoja huo wamefikia uamuzi wa kuzuia kununua sehemu kubwa ya mafuta kutoka Urusi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumzia awamu hiyo mpya ya vikwazo dhidi ya Urusi Kiongozi wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amewasifu viongozi wa mataifa ya kanda hiyo kwa kufikia makubaliano akisema ilikuwa hatua ngumu lakini muhimu kufikiwa.

Wakati hayo yakijiri, Urusi imeendelea na mashambulio yake Mashariki mwa Ukraine hasa katika jimbo la Donbas. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.