Pata taarifa kuu

Vita vya Ukraine vysababisha mgawanyiko ndani ya kundi la Visegrad

Vita vya Ukraine vinabadilisha kadi za uhusiano wa kimataifa, pamoja na nchi za Ulaya. Hungary imefuta mkutano uliopangwa kufanyika Jumatano Machi 30 na Alhamisi Machi 31 huko Budapest baada ya mawaziri wa ulinzi wa Poland na Jamhuri ya Czech kujiondoa kwenye uteuzi huu kwa sababu ya uhusiano wa serikali ya Hungary na Moscow, yote hayo katikati mwa uchaguzi wa wabunge nchini Hungary. Hata hivyo nchi hizi ni washirika katika kundi la Visegrad.

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban (hapa, ilikuwa Februari 12, 2022) haonekani kuwa tayari kukata uhusiano na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban (hapa, ilikuwa Februari 12, 2022) haonekani kuwa tayari kukata uhusiano na Rais wa Urusi Vladimir Putin. REUTERS - BERNADETT SZABO
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Czech alikuwa alitoa taarifa ya kufutwa kwa mkutano huo siku ya Ijumaa: hakuna mkutano huko Budapest na "wanasiasa wa Hungary ambao wanaona kuwa mafuta kutoka Urusi ni muhimu zaidi kuliko damu za raia wa Ukraine". Na ni nani, zaidi ya hayo, wako katikati ya kampeni ya uchaguzi.

Waziri wa Poland alitangaza Jumanne kwamba hatahudhuria mkutano huo. Chama cha upinzani cha Sheria na Haki kilikaribisha uamuzi huo mjini Warsaw.

Kutokana  na Urusi, Waziri Mkuu wa Hungary, bila shaka, amepigia kura vikwazo, lakini anakataa kwamba mafuta kutoka Urusi yalengwe au kwamba silaha zipitie katika ardhi yake kusaidia Ukraine.

Viktor Orban wa Hungary haonekani kuwa tayari kukata uhusiano na Vladimir Putin wa Urusi. Kabla ya Baraza la Ulaya wiki jana, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alikuwa amemtolea wito Viktor Orban kuchagua kambi yake.

Mivutano hii ndani ya kundi la Visegrad inaendelea: Poland na Hungary hadi sasa zimesaidiana mara kwa mara katika kupinga Tume au Baraza la Ulaya kuhusu masuala ya demokrasia na utawala wa sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.