Pata taarifa kuu

Malkia wa Uingereza akutwa na corona baada ya kupimwa

Malkia Elizabeth wa Uingereza amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona hii leo. Kasri la Buckingham limesema, Malkia ana dalili za kawaida kama za mafua.

Malkia Elizabeth II ndiye mfalme wa Uingereza aliyetawala kwa muda mrefu zaidi nchini humo. Hapa, Aprili 19, 2018.
Malkia Elizabeth II ndiye mfalme wa Uingereza aliyetawala kwa muda mrefu zaidi nchini humo. Hapa, Aprili 19, 2018. Toby Melville / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Malkia mwenye umri wa miaka 95, alikuwa akiwasiliana na mtoto wake mkubwa ambaye ndiye mrithi wake, Prince of Wales, ambaye alikutwa na virusi vya Corona wiki iliyopita.

 

 

Inaeleweka kuwa watu kadhaa wamepima virusi katika Windsor Castle, ambako Malkia anakaa.

Kasri la Buckingham limesema kwamba kiongozi huyo ataendelea kufanya shughuli zake nyepesi katika Kasri la Windsor katika kipindi cha wiki chache zijazo na ataendelea kutibiwa na kufuata miongozo yote ya kupambana na maambukizi vya virusi vya Corona.

Malkia Elizabeth tayari amepata chanjo tatu dhidi ya COVID. Malkia alipokea chanjo yake ya kwanza ya Covid mnamo 9 Januari 2021.

Hao yanajiri wakati serikal ya Mkuu Boris Johnson, wiki ijayo itaondoa vizuizi vyote vilivyosalia vya kupambana na maambukizi katika mkakati wake wa "kuishi na virusi vya Corona" pamoja na kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Keir Starmer.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.