Pata taarifa kuu

Montagnier, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba kwa ugunduzi wa VVU, aaga dunia

Luc Montagnier alifariki dunia Februari 8, 2022 katika Hospitali ya Marekani huko Neuilly-sur-Seine. Profesa katika Taasisi ya Pasteur na mkurugenzi wa utafiti katika Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Kisayansi (CNRS), alitunukiwa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 2008 na Françoise Barré-Sinoussi kwa ugunduzi wa virusi vya VVU.

Luc Montagnier wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwaka wa 2017.
Luc Montagnier wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwaka wa 2017. AFP - STEPHANE DE SAKUTIN
Matangazo ya kibiashara

Habari hiyo ilianza kutolea tangu siku ya Jumatano, kwa tangazo, na tovuti ya FranceSoir, kisha na washirika wake wa karibu kwenye Twitter, kuhusu kifo cha Profesa Montagnier.

"Kulingana na vyanzo viwili tofauti, moja ya matibabu, nyingine ya kisiasa, tunaweza kuthibitisha kwamba Luc Montagnier alifariki dunia Jumanne, akiwa na umri wa miaka 89, katika hospitali ya Marekani huko Neuilly. Alipohojiwa na Gzeti la CheckNews, Dk. Béatrice Milbert (ambaye alikuwa na mazungumzo naye kuhusu yeye kuandaa kongamano huko Geneva mnamo Januari 2021) pia alithibitisha kifo chake. Halmashauri ya jiji la Neuilly, hatimaye, ilituthibitishia ilipokea kutoka kwa familia yake cheti cha kifo ", aliandika Alhamisi hii Februari 10 tovuti ya Gazeti kila siku ya Libération.

Katika miaka ya 1980, Luc Montagnier alifanya kazi juu ya saratani zinazosababishwa na virusi katika Taasisi ya Pasteur. Akiwa na watafiti Françoise Barré-Sinoussi na Jean-Claude Chermann, alitenga virusi vya VVU vinavyosababisha UKIMWI. Kwa kujitolea sana katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, Profesa Luc Montagnier aliendelea kupambana na janga hili ambalo limeendelea kusababisha vifo vya mamilioni ya watu duniani kote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.