Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Rais wa Ufaransa akiri kuwepo kwa tofauti ya kisiasa na waziri Mku wa Hungary

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekiri tofauti ya kisiasa na  waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban katika ziara yake jijijni Budapest, huku akisema kuwa bado kuna nia ya kufanya kazi kwa pamoja kwa bara la Ulaya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban wakifanya mkutano na waandishi wa habari huko Budapest, Desemba 13, 2021.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban wakifanya mkutano na waandishi wa habari huko Budapest, Desemba 13, 2021. AFP - ATTILA KISBENEDEK
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo nchini Hungary ilikuwa ya kwanza kwa rais wa Ufaransa tangu mwaka 2007 na ilihusisha mataifa manne ya Jamhuri ya Czech, Hungary, Poland, na Slovakia.

Mara kwa mara Rais Macron amekuwa akisema kuwa waziri mkuu Orban, ni mtu mwenye akili huru.

Waziri mkuu wa Hungary, ambaye Rais Macron alimzungumzia  wiki iliyopita kama mpinzani wa kisiasa, lakini mshirika wa Uala alisema alikubali ufafanuzi wa uhusiano wao.

Sera ya pamoja ya ulinzi wa Ulaya, nishati ya nyuklia, na kilimo yalikuwa masuala matatu kwenye ajenda ya makubaliano yao

Katika ziara hiyo Rais Macron alizuru makaburi ya wayahudi mjini Budapest ambapo aliweka shada la maua kwenye kaburi la mwanafalsafa wa Hungaria Agnes Heller.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.