Pata taarifa kuu

Omicron: Nchi za Ulaya zatakiwa kuagiza raia wao kupokea chanjo ya lazima

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen amesema nchi za Umoja huo zinapaswa kuanza kufikiria, kuagiza watu kupokea chanjo za kukabiliana na virusi vya Covid kwa lazima, ili kupambana na kirusi kipya cha Omicron.

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen katika makao makuu ya Umoja wa Ulaya huko Brussels mnamo Desemba 1, 2021.
Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen katika makao makuu ya Umoja wa Ulaya huko Brussels mnamo Desemba 1, 2021. AFP - KENZO TRIBOUILLARD
Matangazo ya kibiashara

Wito huu unakuja, wakati huu mataifa mengi ya Ulaya yakisitisha safari za ndege kutoka mataifa ya Kusini mwa Afrika.

Hayo yanajiri wakati Ufaransa imeweka kipimo cha PCR kwa msafiri yeyote anayewasili kutoka nchi isiyo ya Umoja wa Afrika.

Wasafiri wanaowasili nchini Ufaransa kutoka katika nchi ambayo si mwanachama  wa Umoja wa Ulaya sasa watalazimika kuwasilisha cheti kinachoonyesha kuwa walifanya kipimo cha PCR, na kukutwa hawana maambukizi yoyote ya virusi vya Corona , ikiwa wamechanjwa au la.

Kutokana na tishio la kirusi kipya cha Omicron, Ufaransa imetangaza Jumatano hii, Desemba 1 kwaamba inaongeza masharti ya kuingia kwenye ardhi yake kwa kuweka hasa kipimo kinachoonyesha kuwa wasafiri wote hawana maambukizi ya virusi vya Corona, hata kama walichanjwa, na ambao wanatoka katika si mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Kwa wasafiri kutoka nchi za Umoja wa Ulaya, Ufaransa itaweka kipimo cha saa 24 kwa watu ambao hawajachanjwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.