Pata taarifa kuu
ITALIA-HAKI

kiongozi wa zamani wa Catalonia Puigdemont kufikishwa mahakamani Italia

Kiongozi wa zamani wa Catalonia Carles Puigdemont, ambaye anakabiliwa na waranti wa Ulaya wa kukamatwa uliotolewa na Uhispania kwa lengo la kuruejeshwa nchini, ameripoti leo Jumatatu mbele ya mahakama huko Sardinia, ambapo alizuiliwa kwa muda wa saa chache Septemba 23.

Carles Puigdemont, 58, mbunge wa Ulaya tangu 2019, Bwana Puigdemont, aliomba mahakama ya Uropa irejeshe kinga yake kama mbunge wa Ulaya kupinga ombi la kurudishwa nchini Uhispania, wakili wake aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa.
Carles Puigdemont, 58, mbunge wa Ulaya tangu 2019, Bwana Puigdemont, aliomba mahakama ya Uropa irejeshe kinga yake kama mbunge wa Ulaya kupinga ombi la kurudishwa nchini Uhispania, wakili wake aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa. François Walschaerts AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Septemba 24 Mahakama ya Rufaa ya Sardinia ilitoa uamuzi wa kusikilizwa kwa kesi hiyo baada ya kukamatwa kwa kiongozi huy wa zamani wa Catalonia alipowasili Alghero, ambapo alipaswa kushiriki katika sherehe ya kitamaduni.

Aliachiliwa siku iliyofuata. Carles Puigdemont, ambaye Uhispania inamshutumu kwa uchochezi na ubadhirifu wa Mali ya Umaa alirudi Brussels ambako anaishi, lakini alijikubalisha kurudi katika kisiwa hiki kikubwa kusini mwa Italia kwa kusikilizwa Jumatatu.

Jaji wa Italia atalazimika kuthibitisha au la uamuzi wa Mahakama ya rufaa ili amwachilie huru. "Wakati wa kusikilizwa, itakuwa muhimu kuamua ikiwa waranti wa Ulaya wa kukamatwa unaweza kutumika au la," wakili wake kutoka Italia, Agostinangelo Marras, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kesi hiyo itachunguzwa na majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, ambao uamuzi wao unaweza kukatiwa rufaa kwa Mahakama ya Cya juu zaidi, ameelezea wakili huyo. "Kwa sasa suala la kurejeshwa Uhispania halitajadiliwa," ameongeza.

Carles Puigdemont, 58, mbunge wa Ulaya tangu 2019, Bwana Puigdemont, aliomba mahakama ya Uropa irejeshe kinga yake kama mbunge wa Ulaya kupinga ombi la kurudishwa nchini Uhispania, wakili wake aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.