Pata taarifa kuu
HUNGARY-JAMII

Waziri mkuu wa Hungary ajitetea kuhusu muswada wa sheria unaokataza maudhui ya ushoga.

Waziri mkuu wa Hungary, Viktor Orban, ametupilia mbali ukosolewaji wa nchi yake kuhusu muswada wa sheria unaokataza maudhui ya ushoga kufundishwa shuleni.

Waziri mkuu wa Hungary Victor Orban wakati wa mkutano na wanahabari juni 2021
Waziri mkuu wa Hungary Victor Orban wakati wa mkutano na wanahabari juni 2021 AFP
Matangazo ya kibiashara

Akiwa mjini Brussels, anakohudhuria kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Ulaya, waziri mkuu Orban, amesema haoni sheria hiyo ikikiuka haki za binadamu badala yake inalinda watoto.

Orban amefahamisha kuwa amekuwa mpigania uhuru wakati wa utawala wa kikomusti na ushoga ulikatazwa na kwamba alipigania uhuru na haki za mashoga.

Waziri mkuu Orban pia amesema analinda haki za watu hao,na kaonyesha kuwa sheria hiyo haihusu ushoga bali ni kuhusu haki za watoto na wazazi wao, sheria tayari imepitishwa na inafanya kazi.

Kiongozi huyo pia ameonya kwamba ni bora kusoma kabla ya kutoa maoni, na huo ndio utaratibu mzuri, amesisitiza Viktor Orban, Waziri mkuu wa Hungary

Matamshi yake Orban yametolewa wakati huu viongozi wenzake, wakiishutumu Hungary, kwa kujaribu kuminya haki za watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.