Pata taarifa kuu
VATICAN-KANISA-HAKI

Vatican yatoa mwongozo wa uchunguzi kuhusu madai ya unyanyasaji wa kijinsia

Katika juhudi za Papa Francis, Vatikani imetoa mwongozo kwa viongozi wa kanisa kuhusu utaratibu unaotakiwa kufuata ili kubaini watuhumiwa wa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto katika Kanisa Katoliki duniani.

Kiongozi wa kanisa Katoliki, Papa Francis.
Kiongozi wa kanisa Katoliki, Papa Francis. VATICAN MEDIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waraka huo ni "chombo" kilichokusudiwa kusaidia viongozi wa Kanisa huko Vatican "katika majukumu magumu ya kutekeleza vilivyo kesi" zinazohusisha viongozi wa kidini "wakati wanashutumiwa kuhusika na" vitendo vya unyanyasaji wa watoto, amesema katika taarifa Kadinali kutoka Uhispania Luis Ladaria Ferrer, mkuu wa kitengo cha Imani katika kanisa Katoliki.

Papa Francis, ambaye ameendelea kufanya mapambano dhidi ya kashfa hii ya unyanyasaji wa kijinsia katika kanisa Katoliki moja ya vipaumbele katika uongozi wake, aliiitisha mkutano mwezi Februari 2019 uliojumuisha viongozi 114 wa mabaraza ya maaskofu duniani.

Katika hafla hiyo walikubaliana "kutoa mwongozo unaofanana kwa kanisa Katoliki, wakitaja viwango wa kisheria ambavyo vinatekelezwa kwa Kanisa hilo

Waraka huo uliotolewa leo Alhamisi haupendekezi hatua mpya badala ya haki ya Kanisa Katoliki kwa utaratibu wa mahakama, imbaini Vatican katika taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.