Pata taarifa kuu
URENO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ureno kuanza kulegeza vizuizi vya kudhibiti Corona Mei 3

Ureno inatarajia kuanza kulegeza vizuizi vya kudhibiti ugonjwa wa Covid-19 Mei 3. Ureno ilichukuwa hatua za kufunga maduka yote na huduma zisizo muhimu kwa kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Corona.

Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa.
Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa. TIAGO PETINGA / LUSA
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo zoezi la kurejesha tena uchumi ni mchakato ambao utachukuwa muda mrefu, Rais Marcelo Rebelo de Sousa amesema.

"Kilicho muhimu katika awamu hii mpya ni kwamba Wareno wanapaswa kujua kuwa kudhibiti (janga hili) bado ni muhimu na kwamba lazima tuchukue hatua ndogo na kutathmini hali hiyo kila wakati," rais wa Ureno ameongeza katika mkutano na waandishi wa habari.

Nchini Ureno hali ya dharura ilitangazwa Machi 18.

Kiasi cha watu milioni 3.03 wameripotiwa kuambukizwa na virusi vya corona duniani kote na watu 210, 263 wamefariki, kwa mujibu wa idadi iliyokusanywa na shirika la habari la Reuters. Maambukizo yameripotiwa katika nchi na majimbo zaidi ya 120 tangu mgonjwa wa kwanza kugundulika nchini China Desemba mwaka 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.