Pata taarifa kuu
UFARANSA-JAMII-MGOMO

Shughuli mbalimbali zaendelea kukwama Ufaransa

Mgomo dhidi ya Mageuzi ya hazina ya uzeeni uneendelea kuzorotesha shughuli mbalimbali nchini Ufaransa. Ni siku kumi na mbili sasa tangu kuzuka kwa mzozo wa kijamii nchini Ufaransa.

Ufaransa yaendelea kukumbwa na mgomo.
Ufaransa yaendelea kukumbwa na mgomo. REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu hii, Desemba 16, usafiri wa umma umezorota, huku watu wakifurika kwenye vituo mbalimbali vya treni na kwenye vituo vya magari.

Madereva wameingia katika mgomo Jumatatu hii, Desemba 16, huku wakitoa madai yao. Vyama vinne vimewataka wafuasi wao waitikie mgomgo huo.

Vyama hivyo vinadai nyongeza ya mshahara lakini pia kuendelea kwa likizo yao ya kumaliza-kazi, ambayo inasababisha madereva wengine kustaafu mapema na wanaweza kutoweka na mageuzi.

Mapema leo asubuhi vizuizi vimewekwa barabarani katika miji ya Lille, Vannes, Toulouse, Lyon, Nancy na Miramas.

Wafanyakazi nchini Ufaransa wanasema hawataki mabadiliko hayo ambayo wanasema yataathiri masiha yao, kuelekea na baada ya kustaafu na namna watakavyopata mafao yao

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.