Usalama: Viongozi wa NATO wakutana kwa mazungumzo London
Viongozi kutoka nchi zinazounda Umoja wa jeshi la kujihami kwa nchi za Magharibi NATO, wanakutana jijini London kujadili masuala mbalimbali ya usalama na ushirikiano kati yao.
Imechapishwa:
Mkutano huu unafanyika nchini Uingereza, siku kumi kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini humo.
Tayari Rais wa Marekani Donald Trump amewasili jijini London, na kuelekea katika mkutano huu amekuwa akijigamba kuwa, tangu aingie madarakani, nchi wanachama wa NATO zimeimarisha uwajibikaji wao, kinyume na ilivyokuwa zamani.
Kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo wa sabini wa NATO, Rais Trump na viongozi wengine wa dunia, watakuwa na dhifa na Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili.
Mbali na mkutano huo wa NATO, viongozi wengine wa dunia kama vile Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wanatarajiwa kukutana pembezoni mwa mkutano huo kujadili ushirikiano kati ya nchi zao.