Pata taarifa kuu
HUNGARY-WAHAMIAJI-USALAMA-HAKI

Wahamiaji: Orban ataka Tume mpya ya Ulaya kuundwa

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban amesema kuwa Tume mpya ya Ulaya inahitajika ili kutekeleza sera mpya ya uhamiaji, akisema muhula wa tume hiyo unakaribia "kumalizika" ifikapo mwezi Mei mwaka ujao.

Angela Merkel (kulia) na Viktor Orban kwa muda mrefu wamekuwa wakitafautiana kuhusu sera ya kuwapa hifadhi wahamiaji Ulaya.
Angela Merkel (kulia) na Viktor Orban kwa muda mrefu wamekuwa wakitafautiana kuhusu sera ya kuwapa hifadhi wahamiaji Ulaya. REUTERS/Axel Schmidt
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwenye redio ya Hungary, Orban ameishtumu tena Tume ya Ulaya, ambayo haipaswi kuadhibu nchi za Umoja wa Ulaya ambazo zinalinda mipaka yao dhidi ya kuwasili kwa wahamiaji.

Hivi karibuni Tume ya Ulaya ilianzisha vita vya kisheria na Hungary kuhusu suala la wahamiaji, kwa kuzingatia kama sheria isio halali sheria mpya za Hungary zinazokandamiza msaada kwa wanaotafuta hifadhi.

Hungary ilifahamishwa na Mahakama ya Umoja wa Ulaya (CJEU) kuwa hitambui sheria hiyo mpya.

Orban amebaini kwamba uamuzi wa Tume ya Ulaya haufai na kwamba muhula wake utamalizika hivi karibuni.

"Tunahitaji tume mpya, mbinu mpya," amesema. "Baada ya uchaguzi wa wa viongozi wa Tume ya Ulaya, tutahitaji tume ambayo haiadhibu nchi kama Hungary ambayo inalinda mipaka yake", ameongeza Bw Orban.

Waziri Mkuu wa Hungary ameendelea kusema kwamba Tume ya Ulaya inapaswa kuadhibu mataifa ambayo yanawaruhusu mamilioni ya wahamiaji kuingia Ulaya kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria za Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.