Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-HAKI

Edouard Philippe: Wafungwa wataoachiliwa huru watatakiwa kufuatiliwa

Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe ametangaza Ijumaa wiki hii kwamba kutaundwa "kitengo maalum" kitakachofuatilia wafungwa magaidi au wenye msimamo mkali wa kidini watakao achiliwa huru baada ya kutumikia kifungo chao.

Edouard Philippe, Waziri Mkuu wa Ufaransa, akiwasilisha mpango mpya dhidi ya ugaidi, huko Levallois-Perret, Ijumaa, Julai 13, 2018.
Edouard Philippe, Waziri Mkuu wa Ufaransa, akiwasilisha mpango mpya dhidi ya ugaidi, huko Levallois-Perret, Ijumaa, Julai 13, 2018. GERARD JULIEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Suala la kufuatilia watu hao ni moja ya changamoto za kupambana na ugaidi nchini Ufaransa. Pia amebaini kwamba kutaundwa ofisi ya taifa mashtaka dhidi ya ugaidi (PNAT) ili kukabiliana na tishio la kigaidi nchini Ufaransa, licha ya upinzani kutoka mahakimu wengi.

Suala la kufuatilia wa wafungwa wa kigaidi au wenye msimamo mkali watakaoachiliwa huru baad aya kutumikia kifungo chao na kuundwa kwa ofisi ya taifa ya mashtaka dhidi ya ugaidi ni moja ya mambo muhimu yaliomo kwenye mpango mpya dhidi ya ugaidi, mpango uliozinduliwa Ijumaa hii Julai 13 na Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe, katika hotuba alioitoa kwenye makao makuu ya Idara ya Usalama wa Ndani (DGSI), mjini Paris.

"Kitengo Maalum" kilichotangazwa kitawekwa katika kikosi kinachohusika na uratibu wa mapambano dhidi ya ugaidi (UCLAT) na kuhusisha idara ya upelelezi katika jela, amesema Waziri Mkuu, wakati ambapo takriban wafungwa 450 wa kigaidi au wenye msimamo mkali wa dini wanatarajiwa kuachiliwa huruifikapo mwishoni mwa mwaka 2019, kwa mujibu wa Edouard Philippe.

Baadhi ya [wafungwa] bado ni tishio, hata baada ya kufungwa kwao na hivyo wanahitaji kufuatiliwa kwa uangalifu

Edouard Philippe, Waziri Mkuu wa Ufaransa amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.