Pata taarifa kuu
MALTA-WAHAMIAJI-USALAMA

Malta yakataa kuruhusu kutia nanga kwa meli inayobeba mamia ya wahamiaji

Nchi ya Malta imesisitiza msimamo wake wa kukataa kufungua lango la bandari yake kuruhusu kutia nanga kwa meli ya shirika moja la kiraia linalohusika na uokoaji wa wahamiaji kwenye bahari ya Mediterranian ambayo ina mamia ya wahamiaji.

Malta inasema wahamiaji hao waliokolewa wakiwa kwenye mipaka ya maji ya Italia na kwamba wao hawapaswi kuwapokea.
Malta inasema wahamiaji hao waliokolewa wakiwa kwenye mipaka ya maji ya Italia na kwamba wao hawapaswi kuwapokea. RFI/Guilhem Delteil
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wahamiaji 629 waliokolewa kwenye pwani ya bahari ya Libya wakiwa wameingia kwenye maji ya nchi ya Italia, lakini wakajikuta pabaya baada ya Serikali ya Italia kukataa kuwapokea na kutaka wapelekwe kwenye nchi nyingine.

Taarifa iliyotolewa na waziri mpya wa mambo ya ndani wa Italia Matteo Salvin, imeitaka nchi ya Malta kutofumbia macho janga la wahamiaji na kukubali kuwapokea mamia ya wahamiaji hao ambao bado wako kwenye meli ya shirika la Ufaransa Aquarius.

Malta inasema wahamiaji hao waliokolewa wakiwa kwenye mipaka ya maji ya Italia na kwamba wao hawapaswi kuwapokea, mvutano ambao sasa unazidisha sintofahamu zaidi kuhusu hata ya wahamiaji hao na msimamo wa Serikali mpya ya Italia dhidi ya wahamiaji.

Serikali mpya ya Italia imesema haitapokea wahamiaji, huku ikizitika nchi nyingine za Ulaya kupokea wahamiaji zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.