Hatma ya Salah Abdeslam kujulikana Jumatatu hii
Mahakama jijini Brussels nchini Ubelgiji ,Jumatatu wiki hii, inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya Salah Abdeslam, mshukiwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea jijini Paris nchini Ufaransa mwaka 2016.
Imechapishwa:
Tayari viongozi wa Mashtaka wanataka Abdeslam na mshtakiwa mwezake Sofiane Ayari kufungwa jela miaka 20 kwa makosa ya kigaidi na kumiliki silaha zilizopigwa marufuku.
Abdeslam ambaye anazuiwa nchini Ufaransa anakokabiliwa na kosa lingine la ugaidi lililosababisha vifo vya watu 130 mwaka 2015, hatakuwa Mahakamani wakati hukumu itakapotolewa.
Mashambulizi ya kigaidi yalioyotokea jijini Paris mwaka 2016 yaliua watu wengi na wengine wengi kujeruhiwa.