Pata taarifa kuu
ISRAEL-EU-USHIRIKIANO

Netanyahu kukutana na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya

Baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa mjini Paris siku ya Jumapili, Desemba 10, Waziri Mkuu wa Israel yuko ziarani Brussels kwa mkutano na Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya.

Baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto), Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu anafanya ziara Brussels ili kukutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya (EU).
Baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto), Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu anafanya ziara Brussels ili kukutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya (EU). REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Benjamin Netanyahu atakutana na mawaziri 28 wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wakati wa chakula cha asubuhi.

Waziri Mkuu wa Israeli anaushtumu Umoja wa Ulayaku wa ni"wanafiki" juu ya shutma dhidi ya uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli.

"Ninaheshimu Umoja wa Ulaya lakini siko tayari kukubali sera ya kuegemea upande fulani kutoka kwa umoja huo," Bw Netanyahu amesema. "Wanashutumu tangazo la rais Trump, lakini hawajashtumu kitendo cha kurusha roketi nchini Israeli," ameongeza.

Netanyahu anaweza kutofutilia mbali wazo la kutambua sehemu ya moja magharibi mwaJerusalem kama mji mkuu wa Israe.

Waziri Mkuu wa Israel huenda akakubali ushawishi kutoka Umoja wa Ulaya lakini kazi itakuwa ngumu, mwanahistoria Frédérique Schillo, amesema. "Anakuja na ushindi mkubwa wa kidiplomasia, ambao ni kutambuliwa kwa Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli. Lakini anakuja Ulaya ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanapinga uamuzi huo wa Marekani juu ya Israel. Kwa hivyo, atakua na kazi kubwa kushawishi washirika wake. Lakini bila shaka, yuko atakua na kazi kubwa, kwani viongozi wa nchi hizi hawako tayari kuunga mkono kutambua jerusalem kama mji mkuu wa Israel. "

Suala jingine ambalo linaonekana kuwa litajadiliwa kati ya Netanyahu na viongozi wa Ulaya katika mkutano wao mjini Brussels ni ukoloni wa Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi. Waziri Mkuu wa Israel pia atazungumia suala la kuwepo kwa Iran nchini Syria na Lebanon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.