Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-UCHUMI

Uingereza kutoa mapendekezo yake kuhusu kujitoa kwa Umoja wa Ulaya

Wiki ya maamuzi kuhusu mazungumzo ya kina ya kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya imeingia. Uingereza na nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanatazamia kuamua kama masharti sasa yamemekamilika ili kuingia katika hatua ya pili ya mazungumzo.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker tarehe 2 Desemba 2017, Twyford.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker tarehe 2 Desemba 2017, Twyford. REUTERS/Peter Nicholls
Matangazo ya kibiashara

Theresa May anatarajiwa leo Jumatatu Desemba 4 Brussels kukutana na rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker na Michel Barnier, msimamizi wa mazungumzo hayo mukatika hali ya kuunda mapendekezo kamili kuhusu masuala matatu: mpaka wa Ireland, hati ya kujitenga na sheria kuhusu raia kutoka pande hizo mbili. Ikiwa maendeleo ya kutosha yatakua yamefanyika, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinaweza kukubali makubaliano kwenye vikao vya Baraza la Ulaya vitakavyofanyika tarehe 14 na 15 Desemba.

Mazungumzo kati ya Uingereza na Umija wa Ulaya yamekua yakiendelea kwa miezi kadhaa na Umoja wa Ulaya umetoa tarehe ya mwisho ambayo ni leo Jumatatu Desemba 4 ili kukamilisha hatua ya kwanza na kuingia hatua ya pili ya mazungumzo.

Tarehe 14 na 15 Desemba, viongozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya natarajia kusema ikiwa mazungumzo ya masharti ya kujitenga na Uingereza yamepiga hatua ya kutosha ili kuruhusu ufunguzi sambaba wa mazungumzokuhusu uhusiano wa kiuchumi kati ya umoja huo na Uingereza.

Baada ya siku kadhaa ya mazungumzo na nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya, lakini pia ndani ya chama chake mwenyewe, Theresa May inaonekana yuko tayari kukubali maombi ya awali ya Umoja wa Ulaya. Lakini bado kuna vizingiti fulani

Kwenye hati ya kujitenga kwa pande hizo mbili, makubaliano yalifikiwa: Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alipata idhni kutoka kwa wabunge wa chama cha Conservative kutoa zaidi ya euro bilioni 50 kama inavyodai Brussels.

Kuhusu suala la mpaka wa Ireland, hata hivyo, mambo mengi hayajakamilishwa, na Dublin inaendelea kudai kuepo na makubaliano ya kutosha ili kuzuia kurudi kwa mipaka ya asili kati ya Irelands mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.