Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Mahakama yaagiza kuzuiliwa kwa wanaharakati wa uhuru Catalonia

Majaji nchini Uhispania, wameagiza kuzuiwa kwa viongozi wawili wa jimbo la Catalonia. Wawili hao ni Jordi Sánchez, anayeongoza bunge la jimbo hilo lakini pia Jordi Cuixart anayeongoza masuala ya kiutamaduni katika jimbo hilo.

Rais wa Catalonia Carles Puigdemont amependekeza kukutana na Waziri Mkuu wa serikali uhispania na aameomba mazungumzo katika miezi miwili ijayo.
Rais wa Catalonia Carles Puigdemont amependekeza kukutana na Waziri Mkuu wa serikali uhispania na aameomba mazungumzo katika miezi miwili ijayo. REUTERS/Ivan Alvarado
Matangazo ya kibiashara

Wamenyimwa dhamana na wanachunguzwa kwa tuhma za uchochezi.

Wakaazi wa jimbo hilo mapema mwezi huu, walipiga kura ya maoni kutaka kujitawala, zoezi ambalo serikali ya Madrid imekataa kutambua.

Hayo yanajiri wakati ambapo muda uliotolewa na serikali kuu ya Uhispania kwa rais wa Cataloni kuweka wazi tangazo lake la uhuru unaelekea kuisha.

Rais wa Catalonia amependekeza kukutana na Waziri Mkuu wa serikali uhispania na aameomba mazungumzo katika miezi miwili ijayo.

Rais wa Catalonia Carles Puigdemont aliwasilisha barua kwa Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy, ili kupata fursa hiyo. Waziri Mkuu wa Uhispania aliikua amemtaka kiongozi wa Catalonia kufafanua nia yake siku ya Jumatatu asubuhi.

Madrid ilikuwa imepanga, ikiwa Bw. Puigdemont atakuwa bado hajaweka wazi tangazo lake la uhuru, itatoa tarehe ya mwisho hadi Alhamisi asubuhi kabla ya kusitisha kujitawala kwa eneo hilo, kulingana na Ibara ya 155 ya Katiba.

Kiongozi wa eneo la Catalonia amesalia na saa chache kabla ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa na serikali kuu kuthibitisha wazi ikiwa ametangaza uhuru au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.