Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Uhispania kuelekea kuchukua uamuzi dhidi ya Catalonia

Rais wa Catalonia amependekeza kukutana na Waziri Mkuu wa serikali uhispania na aameomba mazungumzo katika miezi miwili ijayo.

Rais wa Catalonia Carles Puigdemont aliomba mazungumzo na serikali ya Madrid lakini hilo madrid bado inashikilia msimamo wake.
Rais wa Catalonia Carles Puigdemont aliomba mazungumzo na serikali ya Madrid lakini hilo madrid bado inashikilia msimamo wake. REUTERS/Ivan Alvarado
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Catalonia Carles Puigdemont amewasilisha barua kwa Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy, ili kupata fursa hiyo. Waziri Mkuu wa Uhispania aliikua amemtaka kiongozi wa Catalonia kufafanua nia yake siku ya Jumatatu asubuhi.

Madrid ilikuwa imepanga, ikiwa Bw. Puigdemont atakuwa bado hajaweka wazi tangazo lake la uhuru, itatoa tarehe ya mwisho hadi Alhamisi asubuhi kabla ya kusitisha kujitawala kwa eneo hilo, kulingana na Ibara ya 155 ya Katiba.

Kiongozi wa eneo la Catalonia amesalia na saa chache kabla ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa na serikali kuu kuthibitisha wazi ikiwa ametangaza uhuru au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.