Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Marine Le Pen akubali kushindwa, asema Wafaransa wamekataa kuchagua mabadiliko

Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Ufaransa Bi. Marine Le Pen amekubali kushindwa katika duru ya pili ya Uchaguzi wa urais uliofanyika siku ya Jumapili.

Aliyekuwa mgombea urais nchini Ufaransa Marine Le Pen
Aliyekuwa mgombea urais nchini Ufaransa Marine Le Pen bertrand GUAY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wafuasi wake punde tu baada ya matokeo ya awali kutolewa, yalionesha  kuwa mpinzani wake Emmanuel Macron amemshinda kwa kupata asilimia 65.1 ya kura, Marine aliyepata asilimia 34.9 amesema raia wa Ufaransa wameamua kuendelea na uongozi uliopo.

"Raia wa Ufaransa wameamua kuendelea na uongozi uliozoeleka, hawakuchagua mabadiliko," aliongeza Le Pen.

“Nimezungumza na Macron na kumpongeza kwa ushindi, namtakia kila la heri  katika kutekeleza majukumu mazito yaliyo mbele yake,” aliongeza  Le Pen.

Aidha amesema kuwa sasa ataendeleza siasa za upinzani baada ya kumalizika kwa uchaguzi huouliokuwa na ushindani mkali.

Imekuwa ni mara ya pili kwa mwanasiasa huyu anayeongoza chama cha mrengo wa kulia cha Front Nationale kuwania urais nchini Ufaransa bila mafanikio.

Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2012 na sasa mwaka 2017.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.