Pata taarifa kuu
UHISPANIA

Uhispania yaomboleza kifo cha Mwanamke wa kwanza aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi

Uhispania inaomboleza kifo cha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Carme Chacón, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa na miaka 46.

Marehemu aliyewahi kuwa Waziri wa ulinzi nchini Uhispania Carme Chacón, mwenye nguo nyeupe alipowatembelea wanajeshi wa Uhispania nchini Afganistan mwaka 2008
Marehemu aliyewahi kuwa Waziri wa ulinzi nchini Uhispania Carme Chacón, mwenye nguo nyeupe alipowatembelea wanajeshi wa Uhispania nchini Afganistan mwaka 2008 Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Anakumbukwa sana kutokana na umahiri wa kazi yake lakini kwa ziara aliyofanya nchini Afganistan mwaka 2008 akiwa mja mzito alipokwenda kuwatembelea wanajeshi wa nchi yake.

Chacón alipatikana amefariki dunia nyumbani kwake huku ikishukiwa kuwa huenda tatizo la moyo ndilo lililosababisha kifo hicho.

Alikuwa Waziri wa kwanza wa kike kushikilia wadhifa wa Waziri wa Ulinzi katika historia ya nchi yake.

Kuteuliwa kwake, kulionesha mabadiliko ya utamaduni wa uteuzi nchini humo baada ya kumalizika kwa uongozi wa kijeshi.

Wanasiasa na raia wa Uhsipania wamesema wameshtushwa na kifo cha Waziri huyo wa zamani na wamekuwa wakituma risala za rambi rambi kwa jamaa ndugu na marafiki.

Wakati wa uhai wake, alikuwa mwanasiasa kutoka chama cha Kisosholisti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.