Pata taarifa kuu
UTURUKI-EU-MVUTANO

Mvutano mpya wazuka kati ya Uturuki na EU

Mvutano umeongezeka kati ya Uturuki na nchi kadhaa za Ulaya, ikiwa ni pamoja Uholanzi, Ujerumani, Austria na Uswisi. Hizi ni nchi ambazo zilikataa kuruhusu mikutano ya raia wa Uturuki waishio ugenini kufanyika katika ardhi zao au kushiriki kwa mawaziri wa Uturuki katika mikutano hiyo.

Rais Recep Tayyip Erdogan wakati wa hotuba yake katika mji wa Gaziantep, kusini mashariki mwa Uturuki, Februari 19, 2017.
Rais Recep Tayyip Erdogan wakati wa hotuba yake katika mji wa Gaziantep, kusini mashariki mwa Uturuki, Februari 19, 2017. Yasin Bulbul/Presidential Palace/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Lengo la serikali ya Uturuki ni kuwashawishi raia wake waishio nje ya nchi kupiga kura ya "ndiyo" katika kura ya maoni ambayo inalenga kuimarisha madaraka ya Rais wa Recep Tayyip Erdogan. Upinzani tayari unahofia kwamba Uturuki itarejea katika utawala wa udikteta ikiwa "ndiyo" itapata ushindi

Inaaminika kuwa raia wa Uturuki waishio ugenini wako tayari kupiga kura katika neema ya Recep Tayyip Erdogan. Kwa kutuma mawaziri wake kukutana na raia hao, rais wa Uturuki anapanga kuimarisha nguvu zake na anamatumaini ya kuwashawishi wale ambao bado wanasita kupiga kura ya "ndiyo." Kutokana na na uchunguzi kuhusu kukaribiana kwa kura, kura ya raia wa Uturuki waishiio ugenini inaweza kuwa muhimu.

Hata hivyo, mtu anaweza kujiuliza kama ni moja ya sababu ya kutosha ya Uturuki kuizishtumu Ujerumani na Uholanzi kuwa nchi zenye utawala wa "kifashisti"au kuwa zenye utawala wa kiimla". Yote hayo ni kwa sababu serikali zao hazitaki mikutano ya kisiasa kuhusu nchi nyingine kufanyika katika ardhi zao.

Mbinu za uonevu

Maandamano na matusi yaliyotolewa na viongozi wa Uturuki vinawalenga raia wa Uturuki. Wao ni sehemu ya mbinu ya uonevu. Wanataka kujenga imani kwa raia wa Uturuki kwamba kwamba barani Ulaya bado kuna nchi ambazo zinatumia mambo yaliyopitwa na wakati kama vile ufashisti na tawala za kiimla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.