Pata taarifa kuu
ICC-KENYA-RUTO-SHERIA

Kenya: ICC yafutilia mbali kesi dhidi ya Makamu wa Rais Ruto

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imefutilia mbali Jumanne hii, Aprili 5 kesi dhidi ya Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto.

William Ruto, Makamu wa Rais wa Kenyaa, mbele ya majaji wa ICC, Jumanne Mei 14, 2013.
William Ruto, Makamu wa Rais wa Kenyaa, mbele ya majaji wa ICC, Jumanne Mei 14, 2013. REUTERS/Lex van Lieshout/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na ukosefu wa ushahidi, majaji, "wamekubaliana kufuta mashtaka na kutangaza kwamba watuhumiwa wawili hawahusiki na mashitaka hayo," ICC imesema katika taarifa yake, ikibaini kwamba upande wa mashtaka una haki ya kukata rufaa kwa uwamuzi huo."

Aidha, ICC imeamua pia kwamba mwanahabari Joshua arap Sang, aliyeshtakiwa pamoja na Bw Ruto, hana kesi ya kujibu.

William Ruto alikua anakabiliwa na mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na mauaji, kuhamisha watu kwa lazima na mateso yaliyotekelezwa wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Watu wasiopungua 1,200 waliuawa wakati wa mapigano hayo.

Hata hivyo William Ruto alikana mashtaka hayo. Ruto na wanasheria wake walikua wanataka kesi hiyo itupiliwe mbali kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Mwezi Februari Afisi ya Mwendesha mashtaka ilijaribu kutumia ushahidi wa mashahidi waliokua wamejiondoa katika kesi hiyo, lakini majaji wa Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu walitupilia mbali jambo hilo.

Awali Waendesha mashtaka walibaini kwamba baadhi ya mashahidi walilazimika kujiondoa katika kesi hiyo baada ya kupewa hongo na wengine kufanyiwa vitisho.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) Fatou Bensouda alikiri kwamba kujiondoa kwa mashahidi kumeathiri kesi dhidi ya Ruto lakini amesisitiza kwamba bado kuna ushahidi wa kutosha wa kuendelea na kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.