Pata taarifa kuu
UFARANSA-JACQUES CHIRAC

Jacques Chirac aruhusiwa kuondoka hospitali

Jacques Chirac ameruhusiwa Jumatano hii alaasiri kuondoka hospitali ya jijini Paris ambako alikuwa amelazwa tangu Desemba 9 kutokana na afya yake kuwa mbaya na atasherehekea Krismasi na familia yake mjini Paris, watu walio karibu na rais wa zamani wa Ufaransa waliliambia shirika la habri la Ufaransa la AFP.

Jacques Chirac,rais wa zamani wa Ufaransa katika miaka ya 1995-2007.
Jacques Chirac,rais wa zamani wa Ufaransa katika miaka ya 1995-2007. Reuters/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

"Afya yake inaendelea vizuri", chanzo kilio karibu na rais wa zamani wa Ufaransa kimebaini. "Baada ya kufanya uchunguzi muhimu wa afya yake, Jacques Chirac wiki hii atakua nyumbani kwake na atasherehekea Krismasi na familia yake", mtoto wa rais wa zamani wa Ufaransa, Claude Chirac ameliambia shirika la habri la Ufaransa la AFP.

Tangu mwaka 2007 na alipoondoka katika Ikulu ya Elysée, Jacques Chirac anaishi na mkewe Bernadette katika ghorofa moja jijini Paris karibu na mtaa wa Seine, katika kata ya Quai Voltaire. Kwa mujibu wa waandishi wa habari waliokuwepo Jumatano hii mbele ya nyumba ya rais wa zamani wa Ufaransa, hakuna gari ambalo limeonekana likiingia eneo kunakopatikana nyumba hiyo na idadi ya askari polisi iliyokua karibu na nyumba yake ilipunguzwa Jumatato alaasiri.

Kwa mujibu wa chanzo kilichowasiliana na AFP, Chirac na mkewe huenda wamehamia katika nyumba mpya jijini Paris, karibu mita mia moja na kata ya Quai Voltaire. Taarifa hii haikuthibitishwa wala kukanushwa na wasaidizi wake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wasaidizi wa rais wa zamani waliliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kuwa "Jacques Chirac anaendelea vizuri", wakiongeza kuwa Jacques Chirac, mwenye umri wa miaka 83, atapumzika jijini Paris baada ya kuondoka hospitali na wala hatokwenda likizo nchini Morocco kwa ajili ya siku kuu ya mwisho wa mwaka kama alivyokuwa akifanya miaka ya nyuma.

Jacques Chirac, rais wa Ufaransa tangu mwaka 1995 hadi 2007 aliingizwa hospitali Desemba 9, ili kufanyiwa uchunguzi kiafya, lakini hali yake ilikua haitii wasiwasi", Claude Chirac aliambia AFP Desemba 10.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.