Pata taarifa kuu
UFARANSA-AIR FRANCE-MAANDAMANO

Maandamano ya kuwauanga mkono wafanyakazi wa Air France

Mamia ya watu wameongozana Jumatano hii mbele ya Mahakama ya Bobigny na wafanyakazi wa shirika la ndege la Ufaransa la Air France wanaotuhumiwa kosa la "kumvua na kumchania shati" Mkurugenzi wa rasilimali watu. Wafanyakazi hao wanatazamiwa kuhukumiwa Mei 27.

Maandamano ya kuwaunga mkono wafanyakazi wa Air France wanaofuatiliwa na vyombo vya sheria nchini Ufaransa, Desemba 2, 2015 katika mji wa Bobigny.
Maandamano ya kuwaunga mkono wafanyakazi wa Air France wanaofuatiliwa na vyombo vya sheria nchini Ufaransa, Desemba 2, 2015 katika mji wa Bobigny. KENZO TRIBOUILLARD/AFP
Matangazo ya kibiashara

Waandamanji hao walikua wakisema "shukrani kwa ujasiri wa wenzetu".

Wakati wa mchana, waandamanaji wamefanya mstari mrefu kwa heshima ya kuwaunga mkono watuhumiwa hadi Mahakamani. Wakipiga makofi na kusema "tuhuma dhidi ya ndugu zetu zisitshwe", kabla ya kuzuiliwa na askari polisi wengi, wamebainisha waandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Wafanyakazi watano wanatuhumiwa kuhusika na "vurugu" kwa maafisa wawili wa shirika la ndege la Ufaransa la Air France pamoja na walinzi wa usalama, kando ya mkutano wa kamati kuu ya shirika hilo (CCE) uliofanyika Oktoba 5 kuhusu marekebisho kadhaa, walikua walivaa fulana nyeusi na picha ya kitanga chekungu cha mkono kama ishara ya ngumi ambapo majina yao (Pascal Fabrice, Vincent, Samir na Daudi) yaliwekwa kwenye picha hiyo.

Kama ilivyotarajiwa, mahakama imeweka kesi yao kusikilizwa Mei 27 mwakani.

"Air France haina maoni juu ya utaratibu mahakama unaoendelea", amesema kwa upande wake mwanasheria wa shirika hilo la ndege la Air France. Dominique Mondoloni amejizuia kusema kuhusu taratibu za kinidhamu za ndani, ziliyo wazi, kwa njia ya "kukataliwa kwa vurugu."

Marubani wawili pia wanakabiliwa na utaratibuwa kinidhamu kwa kuwarahisishia waandamanaji kuingia katika ukumbi wa kulikokua kukifanyika mkutano wa Kamati kuu ya Air France (CCE). Wafanyakazi wengine kumi na mmoja wanaotuhumiwa kuvunja vizuizi vya kuingia kwenye makao makuu ya Air France, wamefukuzwa kwa muda wa siku 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.