Pata taarifa kuu
UFARANSA-AIR FRANCE-USALAMA WA ANGA

Air France: vyama vya wafanyakazi vyatoa wito kwa maandamano

Vyama vya wafanyakazi vya shirika la ndege la Air France vimeitisha maandamano Alhamisi wiki hii jijini Paris dhidi ya mpango wa marekebisho ya kampuni yao.

Maandamano ya wafanyakazi wa Air France wakipinga wuamzi wa kuwaweka chini ya ulinzi wafayakazi wenzao watano, Oktoba 12, 2015 katika mji wa Roissy Ufaransa.
Maandamano ya wafanyakazi wa Air France wakipinga wuamzi wa kuwaweka chini ya ulinzi wafayakazi wenzao watano, Oktoba 12, 2015 katika mji wa Roissy Ufaransa. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Mpango huu utajadiliwa katika Kamati kuu ya kampuni hiyo. Mkutano huu ni wa kwanza tangu vurugu kutokea katika shirika hilo la ndege tarehe 5 Oktoba mwaka huu.

Mkutano wa Kamati kuu ya shirika la ndege la Air Farance umeanza saa 3:00 asubuhi katika Wilaya ya XVI, ambapo uongozi wa kampuni hiyo utawasilisha "Sekta hadi sekta, idadi ya nafasi zinazotarajiwa kufutwa" ifikapo majira ya joto 2017, kwa mujibu wa Didier Fauverte, Katibu wa Kamati ya Air France (SGC).

Wakati huo huo wafanyakazi wametolewa wito kuvalia "sare za kazi" na kukusanyika mbele ya jengo la Bunge saa 7:00, dhidi ya mpango huo unaotishia ajira 2,900 na kuunga mkono wafanyakazi wenzao watano wanaokabiliwa na mashitaka kutoka na vurugu ziliyoibuka katika shirika la Air France mwanzoni mwa mwezi Oktoba.

Wafanyakazi hawa watano wanatuhumiwa kuhusika katika shambulio la maafisa wawili wa kampuni ambao walikimbilia wafanyakazi wenye hasira, huku mashati yao yakichanwa. Wafanyakazi hao watahukumiwa Desemba 2, baada ya kusimamishwa kwa muda bila malipo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.