Pata taarifa kuu
UFARANSA-UASALAMA WA ANGA

Wafanyakazi wa shirika la ndege la Air France wajitetea

Wafanyakazi wa shirika la ndege la Ufaransa, Air France wamesema wamekasirishwa na hatua za kupunguza matumizi kwenye kampuni hiyo, hatua ambayo iliwapelekea kukivamia kikao cha baraza la wawakilishi wa wafanyakazi na kuanza kutumia nguvu dhidi ya kiongozi wa shirika hilo.

Wafanyakazi wa shirika la ndege la Air France wafanya mgomo baada ya Shirika la ndege la Ufaransa na lile la KLM kutangaza mpango mpya unaotishia kupunguza ajira za watu elfu 2900.
Wafanyakazi wa shirika la ndege la Air France wafanya mgomo baada ya Shirika la ndege la Ufaransa na lile la KLM kutangaza mpango mpya unaotishia kupunguza ajira za watu elfu 2900. REUTERS/Jacky Naegelen
Matangazo ya kibiashara

Hali hii imejiri baada ya Shirika la ndege la Ufaransa na lile la KLM kutangaza mpango mpya unaotishia kupunguza ajira za watu elfu 2 na 900, mpango unaokuja baada ya marubani wa mashirika hayo kukataa kuongeza muda wa safari zao.

Vyama vinne vya wafanyakazi vimeitisha mgomo wa wafanyakazi wa sekta ya anga kupinga mpango huu mpya.

Polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kuwaokoa wakuu wa mashirika hayo, baada ya kuvamiwa na wafanyakazi wenye hasira, waliotangaza wazi kupinga mpango wa kuongeza saa za kurusha ndege kwa marubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.