Pata taarifa kuu
ULAYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Mgogoro wa wakimbizi katika agenda ya mkutano wa EU

Umoja wa Ulaya unajadili tena Alhamisi wiki hii kuhusu mgogoro wa wahamiaji jijini Luxemburg pamoja na wawakilishi wa nchi jirani ya Syria inayokabiliwa na vita, siku moja baada ya wito wa Ufaransa na Ujerumani kubadili sera za hifadhi kwa wakimbizi barani Ulaya.

FREDERICK FLORIN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri wa Sheria na Mambo ya Ndani, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya watakutana katika mkutano uhusuo " Njia ya Bahari ya Mashariki na nchi za Magharibi za Balkan". Mkutano ambao watashiriki Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Lebanon na Uturuki na nchi za Magharibi za Balkan.

Jumatano mbele ya Bunge la Ulaya mjini Strasbourg, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa François Hollande wametoa wito kwa umoja wa kubadilisha sera za hifadhi za "kizamani" katika bara Ulaya, linalokabiliwa na mgogoro mbaya wa uhamiaji tangu mwaka 1945 lakini pia kuzuia kuendelea kwa "vita" nchini Syria.

Mapokezi ya wakimbizi ambao wameendelea kuongezeka nchini Ujerumani ni " kazi ngumu sana " kwa nchi hiyo " tangu ilipoungana", amerejelea Merkel Jumatano usiku wakati wa majadiliano kwenye runinga ya ya serikali ARD.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.