Pata taarifa kuu
UJERUMANI-WAKIMBIZI-USALAMA-HAKI

Ujerumani yaweza kupokea wahamiaji 1.5 mwaka 2015

Ujerumani inaweza ikapokea wahamiaji hadi milioni 1.5 katika mwaka 2015, takwimu ambayo ni kubwa mpaka sasa kuliko ile iliyotangazwa na serikali, limethibitisha gazeti la kila siku la Ujerumani, Bild Zeitung, kulingana na "hati za siri".

Wahamiaji wakipewa chakula wanapowasili katika kituo cha treni cha Schoenefeld kabla kuhamishwa katika kambi ya wakimbizi. Berlin, Oktoba 5 2015.
Wahamiaji wakipewa chakula wanapowasili katika kituo cha treni cha Schoenefeld kabla kuhamishwa katika kambi ya wakimbizi. Berlin, Oktoba 5 2015. REUTERS/Fabrizio Bensch
Matangazo ya kibiashara

Kila mhamiaji aliyepewa hadhi ya ukimbizi, na hivyo kupewa hifadhi nchini Ujerumani ana haki ya kuleta familia yake, limesema gazeti la kila siku la Ujerumani, Bild Zeitung.

Wakimbizi milioni moja u nusu wanatarajiwa kutafuta hifadhi nchini Ujerumani mwaka huu kwa
mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari.

Makadirio hayo mapya ambayo hayajathibitishwa na serikali ya Ujerumani yanajiri wakati kuna ongezeko la wasiwasi kuhusu uwezo wa Ujerumani kukabiliana na idadi kubwa kama hiyo ya wakimbizi.

Serikali ya Ujerumani inakadiria watu laki nane watatafuta hifadhi nchini humo mwaka huu licha ya kuwa baadhi ya wanasiasa wameonya huenda idadi hiyo ikaongezeka maradufu.

Hata hivyo gazeti la kila siku la Ujerumani, Bild Zeitung, limesema kulingana na “nyaraka za siri” wakimbizi na wahamiaji milioni moja na nusu watawasili mwaka huu nchini Ujerumani.

Kama makadirio haya mapya yatathibitishwa, yatachangia bila shaka kuendelea kuikosoa sera ya Angela Merkel ambayo imetajwa katika vyama wa kihafidhina vinavyomuunga mkono kuwa ya ukarimu wa sana. Lakini raia wanaweza kujizuia kutoa maoni yao kuliko ilivyokuwa wiki chache zilizopita kutokana na kuwasili kwa wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.