Pata taarifa kuu
UJERUMANI-ULAYA-WAKIMBIZI-USALAMA

Wahamiaji: mawaziri wa mambo ya ndani wa EU kukutana Septemba 22

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya wanapanga kukutana Jumanne ijayo, Septemba 22 mjini Brussels kwa mkutano mwingine maalum juu ya suala la mgogoro wa wakimbizi.

Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani na Werner Faymann, Kansela wa Austria, walikutana Jumanne Septemba 15 mjini Berlin.
Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani na Werner Faymann, Kansela wa Austria, walikutana Jumanne Septemba 15 mjini Berlin. REUTERS/Hannibal Hanschke
Matangazo ya kibiashara

Ujerumani, ambayo pamoja na Austria inayotoa wito wa kuandaliwa kwa mkutano wa dharura wa Umoja wa Ulaya juu ya suala hili, imetuhumiwa kuendesha sera "isiyoeleweka" , kwa kufuta sheria za Schengen. Angela Merkel amejitetea kufuatia tuhuma hizo na ametaka kuwepo na mshikamano wa Ulaya.

Ujerumani sasa inajiandaa kupokea kati ya watu 800,000 na milioni moja wanaotafuta hifadhi. Tangu kuanza kwa mgogoro huyo, Berlin imezilaumu nchi za Makedonia na Hungary kwa jitihada zao za kuwazuia wakimbizi, akieleza kuwa nchi hizo zinatakiwa kuwapokea wakimbizi wote, na kwamba Ujerumani iko tayari kupokea mamia ya maelfu.

Hivi karibuni, Ujerumani ilionekana kurejelea kauli yake, kwa kuweka utaratibu wa udhibiti kwenye mipaka yake na nchi jirani hasa Austria. Hali hiyo imesababisha Ujerumani kukosolewa na waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya Czech, na kutaja kuwa sera ya Ujerumani " haieleweki ". Kansela Angela Merkel amesema kuwa kusimamishwa kwa Mkataba wa Schengen lazima tu utarahisisha zoezi la kuurodhesha wakimbizi, lakini mtazamo wa uamuzi huu ni tofauti , ukiangaliwa kiundani.

Mtazamo wa Berlin, sera ya Ujerumani hata hivyo iko wazi na ni yenye kueleweka, kama alivyobaini Kansela mwenyewe, inatakiwa "kurejelea msimamo wa Ulaya" ili kufikia mgawanyo sawa wa wakimbizi miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, na kuandaa utaratibu wa kudhibiti wimbi la wakimbizi wanaoingia barani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.