Pata taarifa kuu
UFARANSA

Rais wa zamani wa Ufaransa Chirac akutwa na hatia ya ubadhirifu wa mali ya umma

Rais wa zamani Mashuhuri wa Ufaransa Jacques Chirac amekutwa na hatia ya kufanya ubadhirifu wa mali za umma na kukosa uaminifu na hivyo kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili cha nje.

®Reuters
Matangazo ya kibiashara

Chirac amekutwa na hatia ya kutenda makosa mawili ambayo aliyatenda akiwa Meya wa Jiji la Paris katika kipindi cha mwaka elfu moja mia tisa tisini hadi elfu moja mia tisa tisini na tano.

Ubadhirifu ambao ameufanya unafikia dola milioni moja nukta nane ikiwemo ni pamoja na gharama za ulipajikodi ambazo hazitambuliki fedha zake zilielekea wapi.

Majaji ambao wanasikiliza kesi hiyo wamemtia hatiani Chirac na kuamua kumhukumu kifungo hicho cha miaka miwili lakini anabahatika kwa kutokwenda jela kwani kifungo chake ni cha nne.

Moja ya sababu kuu ambayo imemnusuru Chirac kukabiliwa na kifungo cha gerezani ni pamoja na matatizo yake ya kiafya ambayo yanamkabili kwa sasa rais huyo wa zamani.

Chirac mwenye umri wa miaka sabini na tisa amehukumiwa kifungo hicho wakati mwenyewe akiwa hayupo mahakamani ambako aliwakilishwa na mtoto wake Anh Dao Traxel.

Mwanahseria wa Chirac kwenye kesi hiyo Georges Kiejman amesems kuwa hukumu ambayo imetolewa haitoathiri imani ya wananchi waliokuwa nayo kwa rais huyo wa zamani wa Ufaransa.

Msemaji wa Chama Cha Upinzani cha Kisoshalisti Benoit Hamon amesema hukumu hiyo imechelewa sana lakini ameongeza kuwa ni ishara ya uwepo wa demokrasia katika nchi ya Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.