Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: Macron amuonya Netanyahu dhidi ya 'uhalifu wa kivita' Gaza

Emmanuel Macron alipaza sauti yake Jumapili hii Machi 24 kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kwa mara nyingine tena akiashiria "upinzani wake madhubuti" dhidi ya uvamizi wa Israel dhidi ya Rafah na kuonya kwamba "uhamisho wa kulazimishwa wa raia utakuwa uhalifu wa kivita".

Emmanuel Macron kisha amemfahamisha Benjamin Netanyahu kuhusu nia ya Ufaransa ya "kuleta kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa rasimu ya azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano".
Emmanuel Macron kisha amemfahamisha Benjamin Netanyahu kuhusu nia ya Ufaransa ya "kuleta kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa rasimu ya azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano". AP - Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mahojiano kwa njia ya simu na mkuu wa serikali ya Israel, kiongozi huyo wa Ufaransa pia amesisitiza wito wake wa "kusitishwa vita mara moja huko Gaza" na kulaani vikali "matangazo ya hivi karibuni ya Israeli kuhusu ukoloni". Israel ilitangaza siku ya Ijumaa kunyakua ardhi ya hekta 800 katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu kwa nia ya kujenga makazi mapya.

"Suluhu ya serikali mbili inabaki kuwa suluhisho pekee"

Rais wa Ufaransa pia amesisitiza "kwamba Israeli ifungue mara moja na bila masharti vituo vyote vya kuvuka hadi Ukanda wa Gaza", haswa eneo la Karni, lenye njia ya moja kwa moja ya ardhini kutoka Jordan, pamoja na bandari ya Ashdo, linaripoti Gazeti la Le Parisien.

Emmanuel Macron kisha amemfahamisha Benjamin Netanyahu kuhusu nia ya Ufaransa ya "kuleta kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa rasimu ya azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano". Na amesisitiza tena kwamba "suluhisho la mataifa mawili linabaki kuwa suluhisho pekee" la "kukidhi mahitaji ya usalama ya Israeli na matarajio halali ya Wapalestina."

Emmanuel Macron pia amezungumza kwa simu Jumapili na Mfalme Abdullah II wa Jordan. Viongozi hao wawili "wamejadili juu ya hali mbaya na hali isiyo ya haki ya kibinadamu huko Gaza", kulingana na Elysée. “Wamesisitiza kwamba kuwaweka raia kwenye hatari ya kufa njaa hakukuwa na haki.”

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant alitarajiwa Jumapili hii mjini Washington, wakati ambapo Marekani pia inaongeza shinikizo kwa Israel kufikia usitishaji vita unaoambatana na kuachiliwa huru kwa mateka pamoja na kuingizwa kwa misaada mingi ya kibinadamu huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.