Pata taarifa kuu

Mapigano Gaza: Vita vya maneneo vyaibuka kati ya Joe Biden na Benyamin Netanyahu

Netanyahu anafanya madhara zaidi kuliko manufaa kwa nchi yake, amesema Joe Biden. Mashambulizi ya ardhini huko Rafah ni "mstari mwekundu" ambao haupaswi kuvukwa, rais wa Marekani ameongeza. Baada ya Marekani kubadili kauli, jibu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Israeli halikuchukua muda mrefu kutolewa.

"Ikiwa rais wa Marekani anataka kusema kwamba maslahi ninayotetea yanakwenda kinyume na matakwa ya Waisraeli walio wengi na kwamba hii inadhuru maslahi ya Israeli, basi, ana makosa katika mambo yote mawili," amesema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
"Ikiwa rais wa Marekani anataka kusema kwamba maslahi ninayotetea yanakwenda kinyume na matakwa ya Waisraeli walio wengi na kwamba hii inadhuru maslahi ya Israeli, basi, ana makosa katika mambo yote mawili," amesema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. © Abir Sultan / AP
Matangazo ya kibiashara

Ukosoaji “wa uwongo na usio na msingi,” ametangaza Waziri Mkuu wa Israeli katika mahojiano na Gazeti la Politico, anaripoti mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul. "Ikiwa rais wa Marekani anataka kusema kwamba maslahi ninayotetea yanakwenda kinyume na matakwa ya wengi wa Waisraeli na kwamba hii inadhuru maslahi ya Israeli, basi, ana makosa katika masuala yote mawili. Ni yote kwa pamoja isipokuwa maslahi binafsi. Idadi kubwa ya Waisraeli wako nyuma yangu na wananiunga mkono,” amesema Benjamin Netanyahu.

Wakati huu, vita vya maneneo vimeibuka kati ya pande hizi mbili. Waziri Mkuu wa Israeli pia anathibitisha kwamba ana "mstari mwekundu" wake: kwamba matukio ya Oktoba 7, 2023 hayawezi kutokea tena. Akiwa amedhamiria zaidi kuliko hapo awali, mkuu wa serikali ya Israel anathibitisha tena kwamba mashambulizi ya ardhini katika mji wa Rafah ambapo karibu watu milioni moja na nusu wa Gaza ni wakimbizi ni muhimu ili kuwashinda Hamas. Ushindi uko "karibu sana," ameliambia Gazeti la kila siku la Ujerumani la Bild. Robo tatu ya vikosi vya Hamas viliangamizwa. Idadi ambayo inawakilisha karibu magaidi 13,000. Na kwa Netanyahu, ni suala la wiki chache za mapigano.

Tumaini lazima litoke baharini

Na wakati vifurushi vipya vya misaada vilisafirishwa kwa ndege jana, Jumapili Machi 10, sasa ni kwa njia ya bahari ambapo chakula lazima kiwasili, kupitia ukanda wa bahari unaounganisha Cyprus na eneo la Palestina. Wakazi walikusanyika kwenye ufuo wa bahari kusini mwa Mji wa Gaza kwa matumaini ya kuona meli. Lakini mafanikio.

Hakika, anaandika mwandishi wetu maalum huko Cyprus, Sophie Guignon, kuondoka kwa meli hii iliyosheheni tani 150 za misaada kuliahirishwa mara kadhaa wikendi hii. Msemaji wa serikali ya Cyprus, Konstantinos Letymbiotis, alitangaza kuondoka kwake karibu Machi 10, lakini meli bado iko kwenye nanga asubuhi ya leo Machi 11. Kisha akataja matatizo ya kiufundi.

Timu zimekuwa zikijiandaa kwa safari hii kwa wiki kadhaa; kuvuka hadi Gaza kutachukua siku mbili kufikia kilomita 370 zinazotenganisha kisiwa cha Cyprus na Ukanda wa Gaza. Wakati huo huo, kwenye bandari ya Larnaca, mamlaka ya Israeli ilitangaza kuwa walikuwa wakikagua mizigo, "kulingana na viwango vyao". Kuzinduliwa kwa ukanda huu wa kibinadamu kwa vyovyote vile ni jaribio kwa Cyprus, taifa hili dogo ambalo lilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2004, na ambalo linajikuta katika kiini cha mvutano wa kimataifa kukabili mgogoro wa kibinadamu ambao haujawahi kushuhudiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.