Pata taarifa kuu

Mvutano waibuka kati ya Israel na Hezbollah, mazungumzo kati ya Israel na Hamas kuendelea

Jeshi la Israel na Hezbollah ya Lebanon wamerushiana makombora usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa huku wajumbe wa Misri wakitarajiwa nchini Israel, kwa matumani ya kuendeleza mazungumzo ya usitishwaji vita na kuachiliwa kwa mateka huko Gaza.

Watu wa Lebanon wakipita karibu na jengo lililoharibiwa na milipuko ya mabomu ya Israeli, huko Kfar Kila, kijiji kilicho kwenye mpaka kati ya Lebanon na Israel, kusini mwa Lebanon, Alhamisi, Aprili 18, 2024.
Watu wa Lebanon wakipita karibu na jengo lililoharibiwa na milipuko ya mabomu ya Israeli, huko Kfar Kila, kijiji kilicho kwenye mpaka kati ya Lebanon na Israel, kusini mwa Lebanon, Alhamisi, Aprili 18, 2024. © AP - Mohammad Zaatari
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Israel limeripoti "makombora mawili yalirushwa" usiku na kundondoka kaskazini mwa Israel kutoka Lebanon na kusema kuwa yalilenga "vyanzo vya mashambulizi haya" kwa mizinga.

Ndege za kijeshi zilipigaa "miundombinu" ya Hezbollah katika eneo la Kfarchouba, jeshi la Israeli limesema katika taarifa fupi.

Kwa upande wake, Hezbollah ya Lebanon, vuguvugu linaloungwa mkono na Iran na mshirika wa Hamas ya Palestina, limedai kuhusika katika taarifa kwa vyombo vya habari kwa mashambulizi haya "yaliyolenga" vikosi vya Israeli mpakani.

Siku ya Jumatano jeshi la Israel lilitangaza kwamba lilifanya "mashambulizi" kusini mwa Lebanon, ambapo Hezbollah inaendesha mashambulizi dhidi ya jeshi la Israel ambalo linapiga ngome za vuguvugu la Kishia linaloshirikiana na Hamas ya Palestina.

Hamas na Israel zimehusika katika vita katika Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miezi sita, ambapo jeshi la Israel linajiandaa kwa operesheni ya ardhini huko Rafah, ngome ya "mwisho" ya Hamas iliyoko kusini mwa eneo hilo.

- Kuharibu au kuachilia mateka -

Miji nchi nyingi na mashirika ya kibinadamu yanahofia, katika tukio la mashambulizi, umwagaji damu katika mji huu ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza unaopakana na Misri, hifadhi kwa karibu Wapalestina milioni moja na nusu.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anabaini kwamba mashambulizi dhidi ya Rafah ni muhimu "kuishinda" Hamas na kuwaachilia mateka zaidi ya mia moja ambao bado wanashikiliwa huko Gaza.

Siku ya Alhamisi, msemaji wa serikali ya Israel David Mencer alitangaza kwamba baraza la mawaziri la vita lilikutana "kujadili njia za kuharibu ngome za mwisho za Hamas."

Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, baraza la mawaziri lilijadili mradi mpya wa usitishwaji vita unaohusishwa na kuachiliwa kwa mateka, kabla ya ziara wajumbe wa Misri iliyopangwa kufanyika leo Ijumaa. Misrei, Qatar na Marekani ndio wasuluhishi kati ya Israel na Palestina.

Kwa mujibu wa tovuti ya Walla, ambayo inamnukuu afisa mkuu wa Israel bila kumtaja, majadiliano hayo yanahusiana zaidi na pendekezo la awali la kuwaachilia mateka 20 wanaochukuliwa kuwa kesi za "kibinadamu".

Kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Ghazi Hamad, kwa upande wake amelihakikishia shirikala habari la AFP kutoka Qatar kwamba shambulio dhidi ya Rafah halitaruhusu Israel kupata "inachotaka", ama kuwaondoa Hamas au kurejesha" mateka.

- "Makubaliano sasa" -

Siku ya Alhamisi, famili za mateka ziliandamana tena mjini Tel Aviv, ili kuweka shinikizo kwa serikali kuwaachilia huru.

Hamas ilitoa video ya mateka Hersh Goldberg-Polin siku ya Jumatano, hatua iliyoonekana na vyombo vya habari vya ndani kama inayolenga, miongoni mwa mambo mengine, kuweka shinikizo kwa Israeli katika mazungumzo.

Pengine akizungumza kwa kulazimishwa, kijana huyu mwenye umri wa miaka 23, raia wa Marekani mwenye asili ya Israel anamshutumu katika video hii Bw. Netanyahu na wajumbe wa serikali yake kwa "kuwatelekeza" mateka.

Siku ya Alhamisi viongozi wa nchi 18, ikiwa ni pamoja na Marekani, Ufaransa, Uingereza na Brazil, walitoa wito kwa Hamas "kuachilia mara moja mateka wote." "Makubaliano yaliyo mezani ya kuwaachilia mateka yataruhusu usitishaji mapigano wa mara moja na wa muda mrefu huko Gaza," taarifa inaongezaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.