Pata taarifa kuu

UNRWA: Bila ufadhili wa Marekani, UNRWA yahitaji ahadi zaidi za kimataifa

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza linakosa msimamo wa 'kutoegemea upande wowote' kisiasa, lakini Israel bado haijatoa 'uthibitisho' wa baadhi ya wafanyakazi' wanaodaiwa kuwa na uhusiano na 'makundi ya kigaidi' kama Hamas, wataalam walioidhinishwa na Umoja wa Mataifa walihitimisha Jumatatu Aprili 22. 

Wafanyakazi wa UNRWA wakiwagawia raia magunia ya unga huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, mwezi Desemba 2023.
Wafanyakazi wa UNRWA wakiwagawia raia magunia ya unga huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, mwezi Desemba 2023. AFP - MOHAMMED ABED
Matangazo ya kibiashara

Shutuma za Tel Aviv kwa kiasi kikubwa zilipunguza kasi ya ufadhili wa kimataifa, imefikia hata baadhi ya nchi kama Marekani kusitisha kabisa. Je, ripoti hii iliyotolewa jana inaweza kusaidia Washington kuanza tena kufadhili shirika hilo?

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani anasema  ameridhishwa na majibu ya Umoja wa Mataifa kwa ukaguzi huu, ambao umeahidi kutekeleza mageuzi yaliyopendekezwa, lakini hii haitabadilisha ufadhili wa Marekani kwa UNRWA katika muda wa kati, dola milioni 350, anaripoti mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten. Kwa zaidi ya mwezi mmoja, Bunge la Marekani limepiga marufuku ufadhili wowote hadi mwezi Machi 2025, ili kuwaridhisha wabunge wa Marekani ambao ni wanaongoza propaganda za kupinga UNRWA, hatua hiyo imesisitizwa tena katika muswada uliopitishwa na Baraza la Wawakilishi siku ya Jumamosi Aprili 20 na ambao unatarajiwa kupitishwa na Bunge la Seneti leo Jumanne.

Vivyo hivyo kwa London. Serikali ya Uingereza ilitangaza, mwezi Januari mwaka huu, "kusitiisha kwa muda ufadhili wowote wa siku zijazo" kwa UNRWA, na Jumatatu 22, wabunge wa kihafidhina walisisitiza kudumisha uamuzi huu, anabainisha mwandishi wetu wa London, Sidonie Gaucher. Uingereza haiwezekani kubadili mawazo yake, licha ya kuchapishwa kwa matokeo ya uchunguzi. Nchi hii inakabiliwa na shinikizo kinzani.

Kama lilivyoripoti Gazeti la Guardian siku ya Jumatatu, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Suella Braverman alitangaza, akiwa amezungukwa na Wabunge kadhaa wa Conservative wanaounga mkono Israeli, kwamba "Hamas ilitumia baadhi ya wafanyakazi wa UNRWA na kwamba itakuwa kinyume cha maadili na aibu kwa serikali ya Uingereza kufadhili shughuli za UNRWA" . Wakati wa ushirikiano wake, Uingereza ililipa sawa na euro milioni 40 kwa shirika la Umoja wa Mataifa, karibu nusu ya ambayo ilikuwa katika misaada ya kibinadamu. Serikali inabaini kwamba misaada ya kibinadamu inaweza kuendelea "kushughulikiwa na matawi mengine ya Umoja wa Mataifa kama vile Mpango wa Chakula Duniani".

Ilipoulizwa ni jinsi gani UNRWA itaweza kukabiliana na upungufu huu katika bajeti yake, inaonekana kwamba jumuiya ya kimataifa inazunguka zaidi na zaidi katika shirika hilo, ikishawishiwa na matokeo ya ukaguzi wa muda uliowasilishwa katikati ya mwezi Machi.

Wafadhili wapya wa kibinafsi

Kwa hivyo Japan imezuia mchango wake wa dola milioni 35, baadhi ya wafadhili wameongeza mchango wao maradufu - Norway, Uhispania au Ireland -, nchi mpya pia zimejiunga na safu ya wafadhili - Ureno au Algeria, ambayo kwa mfano iliahidi dola milioni 15, au Iraq, ambayo ilijitolea kutoa dola milioni 25 - na juu ya yote, na hii ni mpya, mwelekeo umeundwa kuhusu mshikamano kwa watu wa Palestina.

Wafadhili wa kibinafsi wamejitokeza, na kuchangia jumla ya dola milioni 50 tangu mwezi wa Februari. UNRWA kwa sasa ina bajeti ya kutosha kufanya kazi hadi mwisho wa mwezi wa Juni, lakini haifikirii kuwa hii itatosha kufidia ombwe lililosababishwa na kuzuiwa kwa dola milioni 350 za Kimarekani. Ahadi nyingi zaidi za kimataifa zitahitajika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.