Pata taarifa kuu

Marekani yaanza ujenzi wa gati na bandari ya muda Gaza

Marekani imeanza ujenzi wa gati huko Gaza, Pentagon imetangaza hivi punde siku ya Alhamisi, mradi unaonuiwa kuwezesha uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo la Palestina linalikkumbwa na mashambulizi ya anga na kuzingirwa na Israel.

Ndege zilidondosha misaada ya kibinadamu kaskazini mwa Ukanda wa Gaza mnamo Aprili 1, 2024 (picha ya kielelezo).
Ndege zilidondosha misaada ya kibinadamu kaskazini mwa Ukanda wa Gaza mnamo Aprili 1, 2024 (picha ya kielelezo). AP - Abdel Kareem Hana
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na kuchelewa na vizuizi vya Israel kuhusu kupeleka misaada ya kibinadamu kwa njia ya ardhini katika Ukanda wa Gaza uliokumbwa na maafa ya kibinadamu, Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza mapema mwezi Machi ujenzi wa bandari bandia. Meli za kijeshi za Marekani "zimeanza kujenga (...) bandari ya muda na gati baharini," msemaji wa Pentagon Jenerali Pat Ryder amewaambia waandishi wa habari.

Gati hilo linapaswa kufanya kazi kuanzia mwanzoni mwa mwezi Mei na "kila kitu kinakwenda kama ilivyopangwa kwa sasa," amehakikisha msemaji wa Pentagon. Bandari hii ya muda inapaswa kuwezesha meli za kijeshi au za kiraia kushusha mizigo yao. Msaada lazima uwasilishwe na vyombo vya usaidizi wa vifaa kwenye gati kwenye pwani. Mashirika yasiyo ya kiserikali pengine yatakuwa na jukumu la kusambaza misaada hiyo mara tu itakapofikishwa katika eneo hilo, Pentagon ilikuwa tayari imebainisha.

Hakutakuwa na askari wa Marekani ardhini

Maafisa wa Marekani wamesema hatua hiyo haitahusisha "wanajeshi wa ardhini" katika eneo lililoharibiwa na vita la Palestina. Hata hivyo, wanajeshi wa Marekani watakuwa karibu na Ukanda wa Gaza wakati wa ujenzi wa gati hilo, ambalo litasimamiwa na wanajeshi wa Israel. Jeshi la Israel litaingilia kati "kutoa usaidizi wa usalama na vifaa," limesema katika taarifa.

Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali mara kwa mara hutukumbusha kwamba aina hii ya mpango haiwezi kuchukua nafasi ya ongezeko muhimu la kuingia kwa misaada ya kibinadamu kwa kutumia njia ya ardhini, kwa wakazi wenye njaa wanaokabiliwa na uhaba wa vifaa vya matibabu.

Pentagon pia inafuatilia "aina ya shambulio la kombora" ambalo lilisababisha uharibifu mdogo karibu na eneo ambalo msaada unapaswa kutua. "Ni muhimu kutambua kwamba yote haya yalitokea kabla ya vikosi vya Marekani kuanza kuwasilisha vifaa," Pat Ryder amesema.

Cogat, shirika lililo chini ya Wizara ya Ulinzi ya Israel linalohusika na masuala ya kiraia ya Palestina, limesema wanamgambo walirusha makombora ambayo yalilenga eneo lisilojulikana la kibinadamu kaskazini mwa Ukanda wa Gaza siku moja kabla wakati wa ziara ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, bila ya majeruhi yoyote kuripotiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.