Pata taarifa kuu

Hamas yarusha video ya mateka wa Marekani mwenye asili ya Israel katika Ukanda wa Gaza

Hamas imerusha video siku ya Jumatano Aprili 24, ambapo mateka aliyetekwa nyara Oktoba 7 wakati wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas akizungumza. Mtu huyo anayeonekana kwenye video hiyo anajitambulisha kama Hersh Goldberg-Polin. 

Marekani mwenye asili ya Israel Rachel Goldberg, mama wa kijana Hersh Goldberg Polin, mateka wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, ameshikilia picha za mtoto wake wa kiume, mjini Jerusalem, Oktoba 17, 2023.
Marekani mwenye asili ya Israel Rachel Goldberg, mama wa kijana Hersh Goldberg Polin, mateka wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, ameshikilia picha za mtoto wake wa kiume, mjini Jerusalem, Oktoba 17, 2023. REUTERS - Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum wa Jerusalem, Nicolas Falez

Ana nywele ndogo na ndevu fupi, lakini kinachoshangaza ni kwamba anaonekana kakatwa mkono na sehemu ya mkono wake wa kushoto. Anazungumza kwa Kiebrania, anataja jina lake, Hersch Goldberg-Polin, na anajitambulisha: tarehe na mahali pa kuzaliwa, majina ya kwanza ya wazazi wake.

Mateka huyo anasema alikamatwa na kujeruhiwa vibaya Oktoba 7; alishiriki katika tamasha la muziki ambalo mamia ya watu waliuawa. "Hakukuwa na mtu wa kutulinda," amesema.

Katika video hii iliyorushwa hewani na Hamas, kijana huyo anamshambulia Benjamin Netanyahu na serikali yake, akisema kwamba serikali inapaswa "kuona aibu" ya kupuuza hatima ya mateka, aibu ya kukataa nafasi nzuri ya kubadilishana wafungwa na mateka, amesema; aibu kwa mazingira magumu ya utumwa wa watu wanaozuiliwa katika Ukanda wa Gaza.

Kulingana na kijana huyo Mmarekani mwenye asili ya Israel, mateka 70 waliuawa na milipuko ya mabomu ya Israel katika eneo la Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.