Pata taarifa kuu

Gaza: Karibu miili 300 yafukuliwa katika hospitali ya Nasser baada ya jeshi la Israeli kuondoka

Takriban miili 300 imefukuliwa katika kaburi la pamoja katika hospitali ya Nasser huko Gaza. Kulingana na ulinzi wa raia kwenye eneo la tukio, kaburi la watu wengi liligunduliwa baada ya kuondoka kwa jeshi la Israeli mwanzoni mwa mwezi huu.

Watu wanafanya kazi ya kuhamisha miili ya Wapalestina waliouawa wakati wa shambulio la jeshi la Israeli na kuzikwa katika Hospitali ya Nasser, huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, hadi kwenye makaburi mnamo Aprili 21, 2024.
Watu wanafanya kazi ya kuhamisha miili ya Wapalestina waliouawa wakati wa shambulio la jeshi la Israeli na kuzikwa katika Hospitali ya Nasser, huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, hadi kwenye makaburi mnamo Aprili 21, 2024. REUTERS - RAMADAN ABED
Matangazo ya kibiashara

Ulinzi wa raia wa Gaza unaendelea na kazi yake ngumu. Tangu Jumamosi Aprili 20, ulinzi wa raia unasema umefukua karibu miili 300, ikiwa ni pamoja na wazee, wanawake na waliojeruhiwa. Anatarajia kugundua wengine. Mamia ya watu wanaaminika hawajulikani waliko. Miili hii ilipatikana katika kaburi la pamoja kwenye uwanja wa hospitali ya Nasser huko Khan Younes. Je, walikuwepo kabla ya operesheni ya jeshi la Israel au walikuwa wahanga wa operesheni hii?

Jeshi la Israel linakanusha na mauaji haya ya halaiki na linadai kuwa halijazika miili yoyote hiyo. Lakini linasema "lilichunguza" miili ambayo tayari ilizikwa na familia zao ili kuona kama kulikuwa na mateka wa Israeli. Kisha lilirudisha miili hiyo mahali pake.

Miili ilipatikana, mikono imefungwa, chini ya taka

Ulinzi wa raia wa Gaza unazungumzia uwezekano wa kunyongwa. Umoja wa Mataifa unaripoti habari tofauti. Huko Geneva, msemaji wa Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema alishtushwa na habari hii. “Kulingana na ripoti zilizotufikia, waathiriwa walizikwa chini kabisa ardhini, wakiwa wamefunikwa na uchafu. Miongoni mwao, kulikuwa na wazee, wanawake na waliojeruhiwa. Huku wengine wakidaiwa kukutwa wakiwa wamefungwa mikono na kuvuliwa nguo, jambo ambalo ni dhahiri linahusisha ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa na sheria za kibinadamu. Hii inahitaji uchunguzi wa kina. Hatuwezi kuridhika na ripoti nyingine katika vita hivi vya kutisha," Ravina Shamdasani amesema.

Kwa kuzingatia hali iliyopo ya kutokujali, anaendelea msemaji wa Umoja wa Mataifa, "lazima tuanzishe uchunguzi huru wa kimataifa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.