Pata taarifa kuu

Antonio Guterres azuru Rafah kwa lengo la 'kusitisha mapigano' katika Ukanda wa Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amefanya ziara nchini Misri siku ya Jumamosi, Machi 23, na kwa usahihi zaidi kwenye milango ya Ukanda wa Gaza. Antonio Guterres ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas ili kumaliza "uhasama huo". Mkuu wa diplomasia ya Israel amemshambulia vikali, kupitia mtandao wa kijamii wa X.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza kutoka kituo cha mpakani cha Rafah, upande wa Misri, Jumamosi hii, Machi 23, 2024.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza kutoka kituo cha mpakani cha Rafah, upande wa Misri, Jumamosi hii, Machi 23, 2024. AP - Amr Nabil
Matangazo ya kibiashara

Baada ya zaidi ya miezi mitano ya vita, wakati eneo la Gaza likiwa limeharibiwa, idadi ya watu waliokimbia makazi yao, wakikabiliwa na njaa, Antonio Guterres amezuru Jumamosi hii upande wa Misri wa mji wa Rafah, ili kushuhudia "maumivu" ya Wapalestina, wafungwa wa "uhasama usiokuwa na mwisho", amesema.

Ametembelea kituo cha mpakani cha Misri siku moja baada ya kukataliwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano huko Gaza, na kusisitiza juu ya haja ya kukomesha mapigano. "Hamko peke yenu," amewaambia Wapalestina katika taarifa kwa vyombo vya habari, bila hata hivyo kutangaza hatua zozote madhubuti.

Sasa zaidi ya hapo awali, usitishaji mapigano wa haraka wa kibinadamu unahitajika, mapigano yanapaswa kusitishwa. Wapalestina wa Gaza, watoto, wanawake, wanaume, bado wamekwama katika uhasama usio na mwisho. Jamii zilifutwa, nyumba kubomolewa, familia nzima na vizazi viliangamizwa, njaa inawakabili raia. Ramadhani ni wakati wa kueneza maadili ya huruma, jamii na amani. Na ni jambo la kutisha kwamba baada ya mateso mengi, baada ya miezi mingi, Wapalestina wa Gaza wanapitia hali ngumu katika mfungo wa mwezi wa Ramadhani huku mabomu ya Israel yakiendelea kuanguka, risasi zikiendelea kurushwa, misaada ya kibinadamu bado inakabiliwa na vikwazo.

"Hakuna kinachohalalisha mashambulizi ya kutisha ya Hamas ya Oktoba 7. Na hakuna kinachohalalisha adhabu ya pamoja wanayopata raia wa Palestina," anasema Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambaye anatoa wito kwa Hamas "kuwaachilia mara moja mateka wote" waliotekwa nyara wakati wa shambulio lake kubwa katika ardhi ya Israeli.

Bwana Guterres pia ameiomba Israel kufanya "ahadi thabiti" kuwezesha kuingia kwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

Antonio Guterres "amelaumu Israel kwa hali ya kibinadamu huko Gaza, bila kulaani kwa njia yoyote magaidi wa Hamas wanaopora misaada," amesema mkuu wa diplomasia ya Israeli. Na kushutumu: “Chini ya uongozi wake, Umoja wa Mataifa umekuwa shirika la chuki dhidi ya Wayahudi na Israeli. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.