Pata taarifa kuu

Qatar: Israel na Hamas 'haziko tayari kwa makubaliano' ya kusitisha mapigano

Israel na kundi la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina Hamas haziko karibu kufikia makubaliano juu ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza na kuachiliwa kwa mateka, amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, mpatanishi katika mgogoro wa nchi hizi mbili, siku ya Jumanne, Machi 12.

Wapalestina waliokimbia makazi yao, ambao walikimbia makazi yao baada ya mashambulio ya Israeli, walianzisha kambi ya mahema kwenye mpaka kati ya Gaza na Misri, kusini mwa eneo hilo, huko Rafah, Januari 26, 2024.
Wapalestina waliokimbia makazi yao, ambao walikimbia makazi yao baada ya mashambulio ya Israeli, walianzisha kambi ya mahema kwenye mpaka kati ya Gaza na Misri, kusini mwa eneo hilo, huko Rafah, Januari 26, 2024. REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA
Matangazo ya kibiashara

Licha ya mazungumzo mapya mwanzoni mwa mwezi wa Machi mjini Cairo, Marekani, Qatar na Misri, nchi hizo tatu zinazohusika kwa upatanishi, hazikuweza kufikia makubaliano ya usuluhishi kabla ya kuanza kwa mwezi Ramadhani, mwezi mtukufu kwa Waislamu.

"Hatuko karibu na makubaliano, ambayo ina maana kwamba hatuoni pande hizo mbili zikikutana kwa lugha ambayo inaweza kutatua kutokubaliana kwa sasa juu ya utekelezaji wa makubaliano," Majed al-Ansari amesema katika mkutano na waandishi wa habari, akiongeza kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamekuwa yakiendelea, baada ya zaidi ya miezi mitano tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, linaripoti shirika la habari la AFP.

Pande zote "zinaendelea kufanya kazi kupitia mazungumzo ili kufikia makubaliano, kwa matumaini wakati wa mwezi wa Ramadhani," ambao ulianza wiki hii na kudumu kwa mwezi mmoja, Al-Ansari ameongeza. Hata hivyo, amebaini kuwa hakuweza "kupendekeza ratiba" kwa ajili ya makubaliano ya usuluhishi, akibainisha kuwa mzozo bado ni "mgumu" kwenye uwanja wa vita.

Maonyo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa

Siku ya Jumapili, kiongozi wa Hamas, Ismaïl Haniyeh, alihakikisha kwamba vuguvugu la Kiislamu limesalia "wazi kwa mazungumzo". Hata hivyo chanzo kilicho karibu na mazungumzo hayo kililiiambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili "kwamba kutakuwa na kuongeza kasi ya juhudi za kidiplomasia katika siku kumi zijazo" ili kujaribu kupata makubaliano katika nusu ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani. .

Hamas inadai haswa kusitishwa kwa mapigano na kuondolewa kwa wanajeshi wa Israeli kabla ya makubaliano yoyote ya kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa huko Gaza. Israel inaitaka Hamas kutoa orodha kamili ya mateka ambao bado wako hai, lakini Hamas imesema haijui ni nani kati yao "aliye hai au alifariki." Kulingana na Israel, mateka 130 wamesalia Gaza, 31 kati yao wanaaminika kuwa walifariki, kati ya takriban watu 250 waliotekwa nyara mnamo Oktoba 7, 2023.

Ili kupata "ushindi kamili" dhidi ya Hamas, Benjamin Netanyahu alitangaza mashambulizi yajayo ya ardhini kwenye Rafah, mji unaounganishwa kwenye mpaka uliofungwa na Misri ambapo, kulingana na Umoja wa Mataifa, karibu Wapalestina milioni moja na nusu wamekusanyika.

Matarajio haya yameibua maonyo ya mara kwa mara kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, hususan Marekani, mshirika mkuu wa Israel, ambayo imepaza sauti yake katika siku za hivi karibuni kwa kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na kuingia kwa misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.