Pata taarifa kuu

Hamas yarusha video inayoonyesha mateka wawili wa Israel waliotekwa nyara Oktoba 7

Kundi la Hamas kutoka Palestina Hamas limerusha video siku ya Jumamosi ikiwaonyesha mateka wawili wa Israel iliowateka nyara wakati wa shambulio lake la Oktoba 7 kusini mwa Israel na kupelekwa Gaza.

T-shirt ya Aviva Siegel, mateka wa zamani wa Hamas, ikiwa na picha ya mumewe Keith Siegel ambayo bado anashikiliwa na kundi la Hamas kutoka Palestina, Februari 28, 2024 huko Geneva.
T-shirt ya Aviva Siegel, mateka wa zamani wa Hamas, ikiwa na picha ya mumewe Keith Siegel ambayo bado anashikiliwa na kundi la Hamas kutoka Palestina, Februari 28, 2024 huko Geneva. © FABRICE COFFRINI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mateka hao wawili wanajitambulisha kama Keith Siegel, mwenye umri wa miaka 64, na Omri Miran, mwenye umri wa miaka 47. Jukwaa la Familia za Mateka limethibitisha utambulisho wao. Siku ya Jumatano kundi la Hamas lilitusha video ya mateka mwingine wa Israel, Hersh Goldberg-Polin mwenye umri wa miaka 23.

Video hii mpya haina tarehe, lakini Omri Miran, 47, anaonyesha kuwa amekuwa mikononi mwa Hamas kwa siku 202. Siku yake ya 202 kifungoni ni Alhamisi. Hii inakuja katikati mazungumzo, chini ya upatanishi wa Qatar na Misri, kwa nia ya kufikiwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza yanayohusiana na kuachiliwa kwa idadi fulani ya mateka.

Akizungumza kwa kulazimishwa, Omri Miran anaelezea "hali ngumu" kutokana na "mashambulio mengi ya Israel" kwenye Ukanda wa Gaza. Anatoa wito kwa familia yake kuishinikiza serikali kufikia makubaliano na Hamas kuruhusu kuachiliwa kwa mateka. Anasema anatumai kuunganishwa tena na familia yake kwa Siku ya Uhuru wa Israeli mnamo Mei 14.

"Tuko hatarini hapa"

Keith Siegel, 64, anarejelea sherehe za Pasaka - Pasaka ya Kiyahudi ambayo wiki ya sherehe zake inakamilika mwaka huu Jumatatu jioni - na anasema ana "tumaini kwamba kunaweza kutokea jambo zuri" kabla ya kububujikwa na machozi. "Tuko hatarini hapa, kuna mabomu, yanahuzunisha na yanatisha," amesema, kabla ya kutoa wito kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na serikali kujadiliana ili kufikia haraka makubaliano ya kuwezesha kuachiliwa kwa mateka.

Maoni ya mateka yameunganishwa na ujumbe kutoka Hamas, ulioandikwa kwa Kiebrania na Kiarabu na kuelekezwa kwa raia wa Israeli, kama vile "shinikizo la kijeshi halijaruhusu kuachiliwa kwa watoto zenu wanaoshikiliwa", "viongozi wenu [...] bado wanaweka hatarini hatima ya watoto zenu wanaoshikiliwa na jinsi wanavyohisi' au 'fanyeni jambo sahihi kabla hamjachelewa'.

"Uthibitisho huu wa maisha ya Keith Siegel na Omri Miran unaonyesha wazi kwamba serikali ya Israeli lazima ifanye kila linalowezekana ili kufikia makubaliano ya kurejea kwa mateka wote kabla ya Siku ya Uhuru," linasema Jukwaa la familia ya mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.