Pata taarifa kuu

Wanadiplomasia wakutana nchini Saudi Arabia kwa majadiliano kuhusu Gaza

Wanadiplomasia wakuu wa Kiarabu na Ulaya wanatarajiwa katika mji mkuu wa Saudi wikendi hii kwa mkutano wa kilele wa kiuchumi na majadiliano juu ya vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza, duru za kidiplomasia zimesema. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken pia atakuwepo kuanzia leo Jumapili.

Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia (picha ya kielelezo).
Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia (picha ya kielelezo). AP - Nariman El-Mofty
Matangazo ya kibiashara

Kongamano la Kiuchumi la Dunia linafunguliwa Jumapili mjini Riyadh, mbele ya mawaziri wa mambo ya nje wa Saudia, Jordan, Misri na Uturuki, kulingana na mpango wa mkutano huo. Siku ya Jumatatu, kikao kinachohusu Gaza kitawaleta pamoja Waziri Mkuu mpya wa Palestina Mohammed Mustafa, mkuu wa serikali ya Misri Mostafa Madbouly na Sigrid Kaag, mratibu wa misaada wa Umoja wa Mataifa kwa Gaza.

Baada ya ziara yake nchini Lebanon, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Stéphane Séjourné ni miongoni mwa maafisa wa Ulaya ambao watasafiri kwenda katika mji mkuu wa Saudia wakati wa mkutano huo kwa ajili ya majadiliano juu ya vita hivyo vilivyozuka kwa shambulio lisilokuwa na kifani la Hamas mnamo Oktoba 7 dhidi ya Israel. "Majadiliano na wenzao wa Ulaya, Marekani na kikanda kuhusu Gaza na hali ya kikanda yamepangwa mjini Riyadh," chanzo cha kidiplomasia kilisema siku ya Ijumaa.

Kufikia usitishaji mapigano wa kudumu

Malengo ya mkuu wa diplomasia ya Ufaransa ni hasa kufanyia kazi kuachiliwa kwa mateka waliotekwa wakati wa shambulio la Hamas na kufikia usitishaji vita wa kudumu, amesema msemaji wake Christophe Lemoine. Waziri wa Ufaransa atasafiri kwenda Israel na maeneo ya Palestina na anapanga "kusisitiza tena kwa Israeli upinzani wetu kwa uvamizi wa Rafah," Christophe Lemoine amesema, akimaanisha mji wa kusini wa Gaza, ambapo mamia ya maelfu ya Wapalestina wamepata hifadhi, na ambayo inatishiwa na mashambulizi ya Israel kwa lengo la kuangamiza ngome ya mwisho ya Hamas.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anatarajiwa kuwasili Jumatatu kukutana na Bi Kaag na Sheikh Abdullah bin Zayed Al-Nahyan, mwenzake wa Imarati, kulingana na msemaji wa wizara hiyo Sebastian Fischer. "Ziara hiyo italenga kufanyia kazi mambo mengi nyeti ya mzozo katika Mashariki ya Kati, juu ya kusitishwa kwa mapigano na kupiga hatua kuelekea mustakabali wa amani," Sebastian Fischer aliongeza kwa vyombo vya habari siku ya Ijumaa.

"Kama mnavyojua, Mataifa ya Ghuba pia yana jukumu muhimu la kutekeleza hapa," alisisitiza. Jirani ya Saudi Arabia Qatar ni inapatikana ofisi ya kisiasa ya Hamas na nchi hii imefanya upatanishi katika mazungumzo ambayo hadi sasa yameshindwa kupata usitishaji vita wa kudumu na kuachiliwa kwa mateka wengi waliotekwa wakati wa shambulio la Oktoba 7. Kwa upande wake, Saudi Arabia ilisitisha majadiliano juu ya kufufua uhusiano na Israeli baada ya kuzuka kwa vita mnamo Oktoba 7, 2023.

Antony Blinken pia kushiriki mazungumzo

Mkuu wa diplomasia ya Marekani pia atakuwa atahudhuria mkutano huo siku ya Jumatatu na Jumanne hasa "kujadili juhudi zinazoendelea zinazolenga kufikia usitishaji wa mapigano huko Gaza ambao utawezesha kuachiliwa kwa mateka," Wizara ya Mambo y Nje ya Marekani ilisema Jumamosi. Antony Blinken, ambaye ataondoka Jumapili, pia "atasisitiza umuhimu wa kuzuia upanuzi wa kikanda" wa vita ambavyo Israel imekuwa ikiendesha katika Ukanda wa Gaza tangu mashambulizi ya umwagaji damu ya Hamas katika ardhi yake Oktoba 7, kulingana na vyombo vya habari vikinukuu msemaji wa Wizara ya mambo y Nje ya Marekani Matthew Miller. Anapanga pia "kujadili njia za kupata amani ya kudumu katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kupitia njia ya taifa huru la Palestina inayoambatana na dhamana ya usalama kwa Israel."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani pia atashiriki katika mkutano wa mawaziri kutoka Baraza la Ushirikiano la Ghuba, jumuiya ambayo inaleta pamoja nchi sita kwenye Peninsula ya Arabia, ikiwa ni pamoja na Qatar, ambayo ina jukumu la mpatanishi kati ya Israel na Hamas. Pia atakuwa katika Kongamano la Kiuchumi Duniani (WEF) ambalo linafanyika mjini Riyadh Jumapili na Jumatatu na limejitolea kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na mpito wa nishati.

Uhamasishaji wa Uturuki ambao unahofia kurefushwa kwa mzozo

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan pia atazuru Saudi Arabia siku ya Jumapili na Jumatatu. Hatari ya mashambulizi ya Israel huko Rafah na kurefushwa kwa mzozo wa eneo la Gaza kunaisukuma Uturuki kuchukua jukumu muhimu zaidi la kidiplomasia - au angalau kujaribu kufanya hivyo, anaelezea mwandishi wetu huko Istanbul, Anne Andlauer.

Waziri wake wa Mambo ya Nje, Hakan Fidan, ambaye ana ufahamu wa kutosha wa suala hilo akiwa mkuu wa idara ya kijasusi kwa zaidi ya miaka kumi na tatu, yuko katikati ya juhudi hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.