Pata taarifa kuu

UN: Utoaji wa misaada Gaza 'kupitia' ukanda wa baharini bado ni hatari bila makubaliano

Marekani na Umoja wa Ulaya zilitangaza, Ijumaa Machi 8, kuanzishwa kwa ukanda wa baharini kati ya Cyprus na Gaza ili kuwasilisha misaada, hwakati njaa ikitanda katika eneo la Palestina, mpango unaofikiriwa na Umoja wa Falme za Kiarabu. Lakini Umoja wa Mataifa unaonya kuwa kutoa misaada, hata kupitia njia hii, bado ni ngumu na haitakuwa njia ya moja kwa moja.

Jumuiya ya kimataifa inatafuta suluhu la kufikisha misaada Gaza, ikikabiliwa na matatizo na zozi la kudondosha misaada. Hapa, moja ya zoezi hilo kaskazini mwa Gaza, Machi 8, 2024.
Jumuiya ya kimataifa inatafuta suluhu la kufikisha misaada Gaza, ikikabiliwa na matatizo na zozi la kudondosha misaada. Hapa, moja ya zoezi hilo kaskazini mwa Gaza, Machi 8, 2024. AP - Leo Correa
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen anatumai kwamba ukanda huu wa kibinadamu wa baharini, wenye urefu wa kilomita 370, unaweza kuzinduliwa Jumapili Machi 10. Kwa sababu, kutokana na utapiamlo na upungufu wa maji mwilini ambao unatishia Wagaza, zoezi la kudondosha misaada kwa ndege yinaonekana kuwa haina nguvu yoyote na ni hatari: watu 5 waliuawa siku ya Ijumaa Machi 8 na wengine 10 kujeruhiwa na vifurushi vya misaada iliyodondoshwa, mwandishi wetu ameripoti huko New York, Carrie Nooten.

Viongozi wa mpango huu wanatambua kwamba operesheni hii itakuwa "ngumu", lakini wamesisitiza azma yao ya kufanya kazi "kuhakikisha kwamba misaada inatolewa kwa ufanisi iwezekanavyo".

"Ni vigumu kufanya kazi hii haraka"

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu, Martin Griffiths, amekaribisha matangazo haya huku akiendelea kuwa mwangalifu: “Huu ni mwanzo wa mazungumzo. Itakuwa vigumu kufanya kazi hii haraka. Tunajua jinsi ilivyo ngumu kusongesha mifumo hii mbele. Tuliona kilichotokea ufukweni siku nyingine... lakini tunahitaji msaada, popote unapotoka. Bila shaka, tunaendelea kusisitiza kwamba tunachohitaji kwa Gaza ni kusitisha mapigano. Lakini pia tunahitaji njia za ardhini na ufikiaji ndio kipaumbele chetu. Hii ndiyo njia pekee ya kuwa na matokeo halisi. "

Mara tu msaada ulipowasili andarini, Washington kwanza ilipendekeza kuwa lingekuwa jukumu la Umoja wa Mataifa kuisambaza. Hata hivyo, Katibu Mkuu Antonio Guterres amekuwa wazi: bila kusitishwa kwa mapigano, usambazaji wowote wa misaada ni hatari sana kutekelezwa.

Je, jeshi la Israel linahusika na upakuaji wa misaada?

Kuanzia sasa, kwa mujibu wa mpango wa Marekani, pengine ni ni hivyo itkavyokuwa kuwa ni jeshi la Israel ambalo litakuwa na jukumu la kufanikisha upakuaji wa misaada ya kibinadamu inayotumwa kupitia ukanda huu wa baharini, ambao utawekwa kwenye pwani ya kaskazini mwa ukanda wa Gaza, anaripoti mwandishi wetu mjini Jerusalem, Michel Paul.

Hali ambayo inaweza kuwa ya wasiwasi baada ya usambazaji wa hapo awali wa misaada ya kibinadamu inayodhibitiwa na Waisraeli mnamo Alhamisi Februari 29: kitendo cha jeshi la Israe kurusha risasi moja kwa moja kwenye umati wa watu waliokuwa wakisubiri msaada na mkanyagano viliosababisha vifo vya watu 115 na wengine 760 kujeruhiwa, kulingana na Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza.

Kwa sababu wanajeshi elfu wa Marekani wangeweza kutumwa katika eneo hilo, lakini hakuna hata mmoja kwenye ardhi ya eneo la Palestina. Hii ni kama sehemu ya utekelezaji wa shughuli hii kubwa ya ukanda wa baharini, na vile vile kwa pendekezo lingine la Washington: pia ujenzi wa bandari ya muda katika pwani ya Gaza.

Lengo la ukanda wa baharini kati ya mji wa bandari wa Larnaca kwenye kisiwa cha Cyprus na Gaza - kilomita 400 kwa jumla - ni kutoa milo milioni 2 kwa siku. Ahadi hii kubwa inaweza kuchukua karibu miezi miwili ya maandalizi, kulingana na Marekani.

Lakini kuanzia Jumapili hii mradi kama huo, lakini kwa kiwango kidogo zaidi, utajaribiwa na UFalme za Kiarabu.

Wakati huo huo, Ujerumani sasa inajiunga na juhudi za kudondosha vifurushi vya kibinadamu huko Gaza. Mpango ambao shauna hatari. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, hizi ni operesheni zinazoruhusu ongezeko la misaada kwa Gaza baada ya ukaguzi wa usalama wa Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.