Pata taarifa kuu

Gaza: Hali inaweza kuwa 'hatari kwa kukosekana kwa usitishaji mapigano kabla ya Ramadhani (Biden)

Rais wa Marekani Joe Biden ameonya kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa hakutakuwa na makubaliano ya usitishwaji mapigano kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambao unaanza wiki ijayo.

Joe Biden anabaini kwamba kusitishwa kwa mapigano ni muhimu huko Gaza, kwa sababu hali itakuwa "hatari sana" nchini Israeli ikiwa uhasama utaendelea wakati wa mwezi wa Ramadhani, mwezi mtukufu kwa Waislamu, ambao utaanza tarehe 10 au Machi 11.
Joe Biden anabaini kwamba kusitishwa kwa mapigano ni muhimu huko Gaza, kwa sababu hali itakuwa "hatari sana" nchini Israeli ikiwa uhasama utaendelea wakati wa mwezi wa Ramadhani, mwezi mtukufu kwa Waislamu, ambao utaanza tarehe 10 au Machi 11. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

"Tunahitaji kupata msaada zaidi huko Gaza, hakuna visingizio," Joe Biden ameiambia tena Israel siku ya Jumanne, wakati Palestina iko katika mzozo mkubwa wa kibinadamu.

"Ninafanya kazi kwa bidii sana" na mamlaka ya Israeli, amebainisha rais wa Marekani, kabla ya kuanza ziara yake. Joe Biden pia anabaini kwamba kusitishwa kwa mapigano ni muhimu huko Gaza, kwa sababu hali itakuwa "hatari sana" nchini Israeli ikiwa uhasama utaendelea wakati wa mwezi wa Ramadhani, mwezi mtukufu kwa Waislamu, ambao utaanza tarehe 10 au Machi 11. 

"Kwa sasa suluhu iko mikononi mwa Hamas," amewaambia waandishi wa habari kabla ya kuchukua ndege, na kuongeza kuwa Israel "inaonyesha ushirikiano" na kwamba pendekezo "la busara" liko mezani kuhusu kusitishwa kwa mapigano.

Hayo yanajiri wakati wapatanishi wa kimataifa na wajumbe wa Hamas wanaendelea na mazungumzo mjini Cairo nchini Misri, ya kujaribu kufikia makubaliano ya usitishaji vita kwa muda katika Ukanda wa Gaza, kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan mapema wiki ijayo. 

Makubaliano hayo pia yanajumuisha kubadilishana mateka waliosalia na mamia ya wafungwa wa Kipalestina sambamba na usambazaji wa misaadaya kiutu Gaza. Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba wajumbe wa nchi hiyo wamesusia mazungumzo hayo baada ya kundi la Hamas kushindwa kutoa orodha ya mateka ambao bado wako hai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.