Pata taarifa kuu

Vita Gaza: Recep Tayyip Erdogan athibitisha wazi uungaji wake mkono kwa Hamas

Katikati ya vita huko Gaza, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anathibitisha uungaji wake mkono kwa Hamas dhidi ya Israeli bila shaka. Katika hotuba iliyotolewa Jumamosi hii, Machi 9, mkuu wa serikali ya Uturuki amehakikisha kwamba "anasimama kidete" nyuma ya kundi la Kipalestina la Hamas. Tayyip Erdogan anajaribu kuwatuliza wale ambao, ndani ya kambi yake mwenyewe, bado wanamwona kuwa mpatanishi sana na serikali ya Kiyahudi.

Katika hotuba iliyotolewa Jumamosi hii, Machi 9, mkuu wa serikali ya Uturuki Recep Tayyip Erdogan anahakikisha kwamba "anasimama kidete" nyuma ya Hamas.
Katika hotuba iliyotolewa Jumamosi hii, Machi 9, mkuu wa serikali ya Uturuki Recep Tayyip Erdogan anahakikisha kwamba "anasimama kidete" nyuma ya Hamas. AP - Pavel Golovkin
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Istanbul, Anne Andlauer

Hii sio mara ya kwanza, mbali na hilo, kwa Recep Tayyip Erdogan kukataa kusema Hamas kama "kundi la kigaidi" na kuelezea kama "kundi la upinzani". Hii pia si mara ya kwanza kwa yeye kudai kuwa na uhusiano na mrengo wa kisiasa wa kundi la Kipalestina. Lakini rais wa Uturuki hakuwahi kuonyesha uungwaji wke mkono kwa maneno ya wazi kama haya, hadi kufikia kujivunia kuwa Uturuki "imesimama kidete nyuma ya viongozi wa Hamas."

Wiki tatu kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo Tayyip Erdogan anatarajia kutwaa tena miji mikubwa, matamko haya yanaonekana kulenga msingi wake wa uchaguzi. Rais wa Uturuki anakosolewa kwa msimamo unaochukuliwa kuwa dhaifu sana, kwa vitendo zaidi kuliko maneno, kuhusiana na Israeli.

Recep Tayyip Erdogan aibika

Baadhi ya wafuasi wake wamemkasirikia kwa kudumisha, licha ya vita huko Gaza, biashara ya nchi yake na taifa la Kiyahudi. Mnamo Februari 24, katika kampeni ya uchaguzi, bango linalotaka "kukomeshwa kwa biashara ya aibu" liliondolewa mara moja na timu za rais.

Recep Tayyip Erdogan ni wazi ameaibishwa na aina hii ya lawama, lakini anaaini kwamba kususia uchumi na kidiplomasia kwa Israel kutadhuru maslahi ya muda mrefu ya Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.