Pata taarifa kuu

Wanawake wa Afrika Kusini walaani ubakaji wa mateka unaodaiwa kufanywana Hamas

Wanawake walioitikia wito wa Baraza la Kiyahudi nchini Afrika Kusini wameandamana mjini Johannesburg siku ya Ijumaa, Siku ya Kimataifa ya Wanawake, kushutumu madai ya ubakaji na unyanyasaji uliofanywa na Hamas dhidi ya mateka wa Israel huko Gaza, na ukimya wa Rais Cyril Ramaphosa.

"Me Too except for the Jews", wanashutumu waandamanaji hawa huko Johannesburg.
"Me Too except for the Jews", wanashutumu waandamanaji hawa huko Johannesburg. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Takriban wanawake na wanaharakati 200 wameandamana chini ya jua kali chini ya bendera "Me Too except for the Jews". "Tumesikitishwa sana na maovu na ukatili yanaofanywa na magaidi wa Hamas," amesema mmoja wa waandalizi, Gabriella Farbercohen, akimshutumu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kwa unafiki.

Akikumbusha kwamba Mkuu wa Nchi anazungumza mara kwa mara kuhusu suala la unyanyasaji dhidi ya wanawake katika nchi ambayo inakabiliwa na moja ya viwango vya juu zaidi vya ubakaji duniani, Bi Farbercohen amesikitika kwamba "katika siku 154 (za migogoro), hajasema chochoteo, hata kulaani unyanyasaji wa kijinsia ambao wanawake hawa wa Israeli walivumilia. "Hakuna anayesikia sauti za wanawake hawa," Mandy Perez, 33, mama wa mabinti watatu alishiriki maandamano hayo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku Jumatatu, kuna "sababu nzuri za kuamini" kwamba waathiriwa wa shambulio la Hamas nchini Israel mnamo Oktoba 7 walibakwa, kama walivyobakwa baadhi ya mateka walioshikiliwa huko Gaza. Umoja wa Mataifa umekosolewa kwa kuchelewa kujibu shutuma za Israel za ubakaji na unyanyasaji wa kingono zinazolenga vuguvugu la Waislam wa Palestina.

Afrika Kusini, mtetezi wa dhati wa kadhia ya Palestina, ni mojawapo ya nchi zinazokosoa mashambulizi makubwa na mabaya ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza, kulipiza kisasi mashambulizi ya umwagaji damu ya Hamas nchini Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.