Pata taarifa kuu

Uturuki yamrejesha nyumbani balozi wake nchini Israel

Uturuki imetangaza siku ya Jumamosi, Novemba 4, kumuondoa balozi wake mjini Tel Aviv kwa mashauriano, kutokana na Israel kukataa kukubali kusitishwa kwa mapigano huko Gaza.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amethibitisha Jumamosi Novemba 4, 2023 kwamba amevunja mawasiliano yote na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, na Ankara ikatangaza kuwa inamrejesha nyumbani balozi wake, kutokana na mashambulizi yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amethibitisha Jumamosi Novemba 4, 2023 kwamba amevunja mawasiliano yote na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, na Ankara ikatangaza kuwa inamrejesha nyumbani balozi wake, kutokana na mashambulizi yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza. REUTERS - CAGLA GURDOGAN
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Istanbul, Anne Andlauer

Balozi wa Israel nchini Uturuki tayari alikuwa ameondoka nchini wiki mbili zilizopita huku kukiwa na maandamano ya wafuasi wa Palestina na hotuba kali za rais Erdogan dhidi ya taifa la Kiyahudi. Hata hivyo, diplomasia ya Uturuki inaendelea kufanya kazi. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye kwa sasa yuko katika ziara ya Mashariki ya Kati, atazuru Uturuki siku ya Jumapili na Jumatatu.

rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anaendelea kupaza sauti, lakini bado yuko makini na anaamini kwamba nchi yake inaweza na ianapaswa kuchukua jukumu katika kukomesha uhasama kati ya Israel na Hamas.

Kwa upande mmoja, rais wa Uturuki kwa hiyo anmetangaza kwamba Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, sio tena "mhirika" wake - "Nimemfuta," amehakikisha. Kwa upande mwingine, amesema kwamba mkuu wa idaar ya kijasusi nchini Uturuki, Ibrahim Kalin, anaendelea kuwasiliana na Israel na Hamas, na kwamba "haiwezekani kukata kabisa uhusiano na Israel".

Waziri wa Mambo ya Nje, Hakan Fidan - ambaye hadi hivi majuzi alikuwa mkuu wa idara ya ujasusi - ni mhusika mwingine muhimu katika diplomasia hii ya Uturuki katika Mashariki ya Kati. Atakutana na mwenzake wa Marekani Antony Blinken wakati wa ziara yake.

Hata kama juhudi zake zimesalia kutokuwa na mafanikio hadi sasa - kwa suala la mateka au kusitisha mapigano - Ankara haiachi wazo la kuwa mpatanishi, pamoja na mambo mengine, kukomesha ghasia huko Gaza. Kwa muda mrefu, Uturuki inasema iko tayari kuchukuwa "nafasi ya taifa mdhamini" kwa upande wa Palestina, kama sehemu ya suluhisho la mazungumzo na la kudumu la mzozo wa Israel na Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.